Pata taarifa kuu
michezo

Bingwa Garcia kutetea mkanda dhidi ya Morales

Bingwa wa ndondi Danny Garcia anatarajia kuingia ulingoni katika mpambano wa kutetea mkanda wake wa uzito wa kati kwa mara ya pili dhidi ya Erik Morales itakapofika tarehe 20 mwezi ujao katika mpambano wa kwanza Brooklyn baada ya kipindi cha zaidi ya nusu karne kupita.

Bondia Danny Garcia,raia wa Marekani anayetaraji kukipiga na Erick Morales
Bondia Danny Garcia,raia wa Marekani anayetaraji kukipiga na Erick Morales bleacherreport.com
Matangazo ya kibiashara

Garcia,ambaye ni raia wa Marekani atatetea taji ya baraza la ndondi la kimataifa alilotwaa kutoka kwa raia wa Mexico Morales mwezi march na taji ya shirikisho la ndondi kimataifa alilotwaa mwezi uliopita kutoka kwa Muingereza Amir Khan katika mizunguko minne ya mpambano.

Morales,ambaye ana rekodi za mtoano 36 hajashiriki mpambano tangu alipopoteza mkanda baada ya kupokea kichapo kutoka kwa Garcia huko Houston.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.