Pata taarifa kuu
LONDON-OLYMPICS 2012

Sir Chris Hoy awa mwanamichezo wa kwanza toka timu ya Uingereza kupata medali ya sita kwenye mashindano ya Olympic na kuweka historia mpya kwa timu hiyo

Mwanamichezo wa Timu ya taifa ya Uingereza Sir Chris Hoy amefanikiwa kuwa mwanamichezo wa kwanza kwa tumu ya Uingereza kupata medali yake ya sita ya dhahabu kwenye mashindano ya Olympic.

Mkimbiza baiskeli Sir Chris Hoy wa timu ya Uingereza ambaye anakuwa mchezaji wa kwanza wa timu hiyo kuweka rekodi ya kutwaa medali 6 kwenye michuano ya Olympic
Mkimbiza baiskeli Sir Chris Hoy wa timu ya Uingereza ambaye anakuwa mchezaji wa kwanza wa timu hiyo kuweka rekodi ya kutwaa medali 6 kwenye michuano ya Olympic Reuters
Matangazo ya kibiashara

Sir Hoy anakuwa ni mwanamichezo wa kwanza wa timu ya Uingereza kuweka historia kwenye mashindano hayo kwa kufanikiwa kutwaa medali yake ya sita kwenye mchezo wa kuendesha baiskeli.

Sir Hoy amefanikiwa kuipiku rekodi ya mwanamichezo miwngine wa Uingereza Sir Steve Redgraves ambaye yeye alifanikiwa kupata medali tano za dhahabu kwenye mashindano ya olympic.

Sir Hoy mwenye umri wa miaka 36 amesema licha ya umri kumtupa mkono lakini amefarijika sana kuweza kutwaa medali hiyo na kwamba watu wengi walidhania hawezi kushinda kwenye mashindano ya mwaka huu.

Mwanamichezo huyo pia amedokeza kuwa huenda akashiriki michuano ya Olypmic ya mwaka 2016 iwapo akiwa na afya njema na pengine akaweka rekodi nyingine kwenye mashindano yajayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.