Pata taarifa kuu
LONDON-OLYMPICS 2012

Wanamichezo 7 toka Cameroon wametoweka kwenye kambi yao mjini London Uingereza

Wanamichezo saba raia wa Cameroon wameripotiwa kutokomea kusikojulikana wakati wakiwa kwenye kijiji cha mazoezi kushiriki mashindano ya mwaka huu ya Olympic yanayofanyika mjini London, Uingereza.

Wanamichezo wa Cameroon wakiingia wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Olympic
Wanamichezo wa Cameroon wakiingia wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Olympic Reuters
Matangazo ya kibiashara

Awali taarifa za kupotea kwa wanamichezo hao zilikuwa kama uvumi lakini safari huu mkuu wa msafara wa wanamichezo toka nchini Cameroon, David Ojong amethibitisha kutoweka kwa wanamichezo wake.

David Ojong, amesema kuwa miongoni mwa wanamichezo waliotoweka kwenye kambi yao ya mazoezi ni pamoja na wanamasumbwi watano na mlinda mlango mmoja wa timu ya taifa ya wanawake.

Maofisa usalama nchini Uingereza tayari wameanza msako dhidi ya wanamichezo hao na kuahidi kuendelea kuwasaka mpaka pale ambapo watapatikana,.

Hili ni tukio jingine kutokea kwenye michuano ya mwaka huu ambapo kumeripotiwa kutoweka kwa wanamichezo wawili raia wa Ethiopia ambao nao waliamua kubakia barani ulaya kwasababu zilizoelezwa kuwa ni zakiuchumi.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.