Pata taarifa kuu
CECAFA

Mashindano ya CECAFA kutimua vumbi Jumamosi hii jijini Dar es Salaam Tanzania

Mashindano ya soka ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati yanaaza Jumamosi hii katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam nchini Tanzania.

Cecafa
Matangazo ya kibiashara

Vilabu 11 vinashiriki katika Makala ya mwaka huu ikiwemo Klabu ya Vita FC iliyopata mwaliko kutoka katika Jamhuri ya Kidemokarsia ya Kongo.
 

Wau Salam ya Sudan Kusini nayo itakuwa inashiriki katika kinyang'anyiro hiki kwa mara ya kwanza na hivyo ni timu itakayokuwa inaangaziwa sana katika mashidnano haya.
 

Mabingwa watetezi Yanga watacheza mchuano wa ufunguzi dhidi ya Atletico ya Burundi huku Wau Salam wakicheza na na APR ya Rwanda.
 

Siku ya Jumapili,Simba ya Tanzania itacheza na URA ya Uganda ,huku Vita club ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ikicheza na AS Ports ya Djibouti.
 

Mashindano hayo yatamalizika tarehe 28 mwezi huu.
Timu zitazoshiriki ni pamoja na

KUNDI ‘A’:
1. Simba [Tanzania ]
2. URA [Uganda)]
3. AS Vita Club [DR Congo]
4. AS Port [Djibouti]
 

KUNDI ‘B’:
1. Azam [Tanzania ]
2. Mafunzo [Zanzibar]
3. Tusker [Kenya]
 

KUNDI ‘C’:
1. Young Africans [Tanzania ]
2. APR [Rwanda]
3. Wau Salam [Sudan Kusini ]
4. Atletico [Burundi]
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.