Pata taarifa kuu
UINGEREZA-USWISS

FIFA yatangaza matumizi ya teknolojia kubaini iwapo goli lililofungwa ni halali au la

Bodi ya Kimataifa ya Chama Cha Soka Duniani imeridhia hatua ya kutumika kwa teknolijia ya kubaini iwapo goli limefungwa au la kutokana na kuwepo kwa utata wa mara kwa mara yanayochangiwa na makosa ya kibinadamu.

Goli lililokataliwa kwenye Komba la Dunia mwaka 2010 lililofungwa na Frank Lampard kwenye mchezo kati ya Uingereza na Ujerumani
Goli lililokataliwa kwenye Komba la Dunia mwaka 2010 lililofungwa na Frank Lampard kwenye mchezo kati ya Uingereza na Ujerumani
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huo umepitishwa baada ya kuwepo kwa makosa kadhaa ya mara kwa mara kwenye maamuzi ya kutambua goli pindi mpira unapoamuliwa iwapo kama umevuka mstari au la na kuzua malumbano makali.

Rais wa Shirikisho la Soka Duniani FIFA Sepp Blatter amesema uamuzi huo wa kutumia teknolijia kuamua iwapo mpira umevuka mstari au la umechangiwa na mzimu wa goli lililokataliwa la Frank Lampard kwenye Kombe la Duniani mwaka 2010.

Bodi ya Kimataifa ya Chama Cha Soka Duniani ilipiga kura na kuamua kwa pamoja kuanzisha matumizi hayo ya teknolijia kwa ajili ya kuepukana na makosa ya kibinadamu katika kuamua mpira kama umevuka mstari au la.

Blatter amekiri aliposhuhudia goli la Lampard lilipokataliwa kwenye mchezo kati ya Uingereza na Ujerumani akasema haiwezi kuvumilia kuona makosa kama hayo yanaendelea kujitokeza na lazima hatua zichukuliwe.

Rais huyo wa FIFA amekwenda mbali na kusema baada ya Kombe la Dunia la mwaka 2010 wakaridhia kuanza mchakato wa kukabiliana na makosa hayo ya kibinadamu na hatimaye sasa wamepata suluhu ya uhakika.

Wakati teknolojia hiyo ikipigiwa chapuo na FIFA kwa upande wake Rais wa Chama Cha Soka barani ulaya EUFA Michel Platini anapinga hatua hiyo na kusema itachangia kuchelewesha mchezo wa soka.

Platini ameongeza kuwa mchezo wa mpira wa miguu utakapoanza kuamuliwa kwa kutumia teknolojia ni lazima utamu wake utapungua na hata kufanya mchezo huo upooze kwani itafika kipindi hata mchezaji akizidi itabidi uamuliwe kwa teknolojia.

Uingereza kupitia Chama Cha Soka FA imesema itakuwa ya kwanza kuanza kutumia teknolojia hiyo ili kuona kama inaweza kusaidia kumaliza utata huu wa magoli ambayo yanafungwa na kukataliwa kwa sababu ya makosa ya kibinadamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.