Pata taarifa kuu
UINGEREZA

Stuart Pearce aeleza sababu za kumuweka kando ya kikosi chake kitakachoshiriki Olimpiki David Beckham

Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Muungano wa Uingereza kwa upande wa mpira wa miguu Stuart Pearce ametoa sababu za kumuweka kando kwenye kikosi chake Kiungo wa Klabu ya Los Angeles Galaxy ya Marekani David Beckham.

Matangazo ya kibiashara

Pearce amesema sababu ambazo zimemsukuma kumuweka kando Beckham kwenye kikosi cha Muungano wa Uingereza ni za mchezo wa mpira wa miguu na akasisitiza hawezi kumchagua mchezaji wa shinikizo la watu wengine.

Timu hiyo ya wachezaji kumi na nane itakayoshiriki mashindano ya Olimpiki baadaye mwezi huu katika Jiji la London haitakuwa na mkongwe Beckham kitu ambacho kimezusha gumzo nchini humo.

Kocha Mkuu wa Timu ya Soka ya Muungano wa Uingereza Pearce amesema yupo sawa na ana uhakika kikosi chake kitafanya vizuri kabisa licha ya kumkosa Beckham ambaye amekuwa akipigiwa chepuo ya kuwepo.

Pearce kama hiyo haitoshi amesema kuwa Beckham hatokuwa sehemu ya makocha wa timu ya taifa kwa sababu wamepewa nafasi saba ambazo zimeshachukuliwa na watu ambao wameteuliwa kwa ajili ya kazi hiyo.

Kwa upande wake mchezaji wa Kimataifa wa zamani wa Wales ambaye anasukuma gozi kwenye klabu ya Manchester United ambaye amejumuishwa kwenye kikosi hicho Ryan Giggs amesema kumkosa Beckham ni kosa kubwa sana.

Giggs, Micah Richards na Craig Bellamy ni wachezaji watatu ambao wanaumri zaidi ya miaka ishirini na tatu ambao wamejumuishwa kwenye kikosi na Kocha Mkuu Pearce wakiwa na jukumu la kishinda medali ya dhahabu.

Kwa upande wake Mkuu wa Chama Cha Olimpiki Cha Uingereza BOA Andy Hunt naye amesikitishwa na hatua ya kuwekwa kando kwa Beckham na amekiri alistahili kumuijshwa kwenye timu ya mpira wa miguu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.