Pata taarifa kuu
MISRI-TANZANIA

Shirikisho la kandanda Misri EFA lataka mechi na Ngorongoro Heroes ya Tanzania.

 Shirikisho la kandanda nchini Misri (EFA) limeomba mechi mbili za kirafiki kati ya kikosi chao cha vijana wenye umri chini ya miaka 20 dhidi ya Ngorongoro Heroes ya Tanzania.

Kikosi cha timu ya vijana wa Tanzania Ngorongoro Heroes
Kikosi cha timu ya vijana wa Tanzania Ngorongoro Heroes sufianimafoto.blogspot.com
Matangazo ya kibiashara

 

Shirikisho hilo limetuma maombi na kutaka mchezo huo kupingwa july 3 na july 5 mwaka huu kwa masharti maalum ikiwa Misri itakuywa mwenyeji wa mechi hiyo watagharamia malazi,chakula na usafiri wa ndani na eneo la mazoezi kwa wachezaji wa Ngorongoro na kama ikiwa mwenyeji itakuwa Tanzania gharama hizo zitakuwa juu ya Shirikisho la kandanda nchini Tanzana,TFF.

Hata hivyo uongozi wa Shirikisho la kandanda nchini Tanzania unajaribu kutathimini gharama za mechi hizo ili kubaini kama itazimudu ndipo itoe maamuzi ya wapi mechi hiyo ichezwe.

Ngorongoro Heroes ilitamba katika mzunguko wa pili wa michuano ya vijana ya Afrika na kufuzu baada ya kuichabanga Sudan 4-3,na sasa wanasubiri fainali za michuano hiyo itakayochezwa Algeria mwaka ujao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.