Pata taarifa kuu
Euro 2012

Mashindano ya soka ya kutafuta ubingwa wa Ulaya kuanza Ijumaa hii huku Uingereza ikipata pigo

Mashindano ya mwaka 2012 ya mchezo wa soka kusaka ubingwa wa bara la Ulaya yanaanza Ijumaa hii nchini Poland.

Matangazo ya kibiashara

Wenyeji Poland wanafungua dimba dhidi ya Ugiriki katika uwanja wa taifa wa Warsaw katika mashindano hayo yanayoyakutanisha mataifa 16.

Poland imejumuishwa katika kundi moja na Urusi na Jahmuri ya Czech ,kipute ambacho Uhispiania ambao ni mabingwa watetezi wanasema wanataka kunyakua tena ubingwa huo baada ya kuishinda Ujerumani mwaka 2008.

Haya ndio mashindano ya kwanza kuandaliwa na mataifa mawili ambapo Ukraine watafungua mchuano wao dhidi ya Sweden siku ya Jumatatu juma lijalo na wamejumuishwa katika kundi moja na Ufaransa na Uingereza.

Wakati hao yakijiri,  Uingereza imepata pigo  baada ya mshambulizi wake Jermain Defoe baada ya kifo cha babake, suala ambalo linampa kocha Roy Hogdson wakati mgumu kwani mshambulizi  mwingine Wayne Rooney hatashiriki katika michuano miwili ya kinyanganyiro hicho. 

Mashindano haya pia yanakumbwa na hofu ya kutokea kwa hofu ya visa vya ubaguzi wa rangi kujitokeza suala ambalo shirikisho la mchezo huo barani Ulaya UEFA linaonya kuwa yeyote atakayepatikana kumbagua mwezake uwanjani au nje ya uwanja atachukuliwa hatu kali za kinidhamu .

Mario Baloteli mchezaji wa kimataifa wa Italia ambaye pia anacheza soka ya kulipwa nchini Uingereza amethibitisha kuondoka uwanjani ikiwa atadhalalishwa na mashambiki au wachezaji wa timu pinzani.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.