Pata taarifa kuu
ULAYA

UEFA yasema haitabadili sheria ya kadi za njano hadi baada ya miaka mitatu

Chama Cha Soka Barani ulaya UEFA kimesema sheria yake ya kadi za njano katika Mashindano ya ngazi za Klabu hazitabadilika katika kipindi cha miaka mitatu Chama hicho kimethibitisha licha ya wachezaji saba kisheria kutakiwa kukosa Fainali ya Ligi ya Mabingwa mwaka huu.

Nahodha wa Chelsea John Terry akipewa kadi nyekundu kwenye mchezo dhidi ya Barcelona baada ya kumpiga Sanchez mgongoni
Nahodha wa Chelsea John Terry akipewa kadi nyekundu kwenye mchezo dhidi ya Barcelona baada ya kumpiga Sanchez mgongoni
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi wa UEFA umetolewa baada ya Fainali ya Klabu Bingwa Barani Ulaya mwaka huu ambayo itafanyika tarehe 19 ya mwezi May kushuhudia wachezaji sita watatu kutoka Chelsea na watatu wa bayern Munich kuwa na kadi mbili za njano hivyo kukosa mchezo huo.

Msemaji wa UEFA amesema hakuna sheria mpya ambazo zitatumika ili kuzifuta kadi hizo za njano kwa hiyo wachezaji hao sita watakosa mchezo huo utakaopigwa katika Dimba la Allianz Arena maskani ya Bayern Munich.

Wachezaji ambao watalazimika kuwa mashabiki kwenye mchezo huo wa Fainali ya Ligi ya mabingwa Barani Ulaya ni pamoja na Raul Meireles, Branislav Ivanovic na Ramires wakati Bayern Munich itawakosa Luiz Gustavo, David Alaba na Holger Badstuber.

Mkuu wa Masuala ya Sheria za UEFA Michael Van Praag amesema bado kuna miaka mitatu kwa ajili ya kutekelezwa kwa mapendekezo na sheria zinazotumika kwa ngazi za Klabu barani ulaya na kama kutahitajika mabadiliko basi yatakuja baada ya kipindi hicho.

Mchezaji mwingine ambaye atakosa Fainali za Klabu Bingwa Barani Ulaya msimu huu ni Nahodha wa Chelsea John Terry ambaye alizawadiwa kadi nyekundu katika mchezo wa pili wa nusu fainali dhidi ya Barcelona katika uwanja wa Nou Camp.

Licha ya Terry kutoruhusiwa kucheza mchezo huo wa Fainali huko nchini Ujerumani amepewa ruhusa wa kuinua Kombe iwapo timu yake itafanikiwa kuwafunga Bayern Munich ambao watakuwa wanacheza kwenye uwanja wa nyumbani.

Sheria hii pia inaweza kuwa msumari kwenye Mchuano wa Kombe la Mataifa ya Ulaya ambao utafanyika nchini Poland na Ukraine kwani mchezaji atakayepewa kadi nyekundu kwenye robo fainali au nusu fainali atakosa mchezo wa fainali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.