Pata taarifa kuu
Klabu Bingwa

Bayern munich kucheza fainali na Chelsea

Real Madrid imeshindwa kuwika  ikiwa katika uwanja wa nyumbani wa Bernabeu Jumatano jioni, na kukubali kichapo dhidi ya Bayern Munich ya Ujerumani, ambao hatimaye walipata ushindi wa magoli 3-1 kupitia mikwaju ya penalti, wakati timu hizo zilipokutana katika mechi yao ya pili ya nusu fainali ya klabu bingwa barani Ulaya.

Wachezaji wa klabu ya Bayern kutoka Ujerumani wakisherehekea ushindi
Wachezaji wa klabu ya Bayern kutoka Ujerumani wakisherehekea ushindi REUTERS/Susana Vera
Matangazo ya kibiashara

Bayern Munich ya Ujerumani, ikichezea uwanja wake wa nyumbani, sasa itaipokea Chelsea ya Uingereza katika fainali ya klabu bingwa barani Ulaya.

Real ilikuwa imeachwa nyuma kwa bao moja katika mechi ya kwanza ya nusu fainali, mechi iliyokwisha kwa Bayern kushinda 2-1, lakini magoli mawili ya Christiano Ronaldo, la kwanza likiwa la penalti katika dakika ya 6, na la pili akiutambariza mpira wavuni dakika ya 14, yaliwapa mashabiki wa Real matumaini ya kufuzu kuingia fainali.

Lakini Arjen Robben alikitia kitumbua cha Real mchanga, wakati naye alipofanikiwa kutandika mkwaju wa penalti hadi wavuni katika dakika ya 27.

Kukosekana kwa mabao zaidi katika muda wa kawaida wa dakika tisini, na hata baada ya dakika thelathini za ziada, kulimaanisha mikwaju ya penalti, na Bastian Schweinsteiger hakushindwa kuielekeza timu yake ya Bayern kwa fainali ya uwanja wa nyumbani.

Kipa Manuel Neuer alifanya juhudi kubwa, akizuia mikwaju miwili ya Real ya Ronaldo na Kaka, huku Mario Gomez na David Alaba wakiendelea kuifungia Bayern.

Hii ilikuwa ni mara ya pili pia kwa Ronaldo kukosa kufunga mkwaju wa penalti katika mechi za klabu bingwa, wakati alipokuwa akiichezea Manchester United, na katika fainali dhidi ya Chelsea mwaka 2008.

Fainali ya klabu bingwa itachezwa siku ya Jumamosi, tarehe 19 Mei.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.