Pata taarifa kuu
BAHRAIN

Mashindano ya magari yaendayo kasi yaliyopangwa kufanyika nchini Bahrain huenda yakahamishwa kwa sababu za Usalama

Chama kinachosimamia Mashindano ya Magari yaendayo kasi duniani maarufu kama Langalanga Formula One inatarajia kuyahamishia mashandinano yanajayo yaliyopangwa kufanyika nchini Bahrain huko China baada ya maandilizi yake kutawaliwa na machafuko.

Dereva Michael Schumacher na Mark Webber wakiwa kwenye Mbio za mwaka 2010 zilizofanyika nchini Bahrain
Dereva Michael Schumacher na Mark Webber wakiwa kwenye Mbio za mwaka 2010 zilizofanyika nchini Bahrain
Matangazo ya kibiashara

Taarifa ambayo imetolewa na Formula One zimesema kuwa kutokana na Wanaharakati nchini Baharain kuendelea kukabiliana na serikali kitu ambacho kinatajwa kitakwamisha shughuli za maandalizi hayo ya mashindano hayo.

Wanaharakati wameitisha maandamano yaliyopewa jina na siku za hasira kuendelea kukabiliana na serikali kitu ambacho kimezifanya kampuni za magari zinazoshiriki kuhofia hali ya usalama wao huko Bahrain.

Timu ambazo zinashiriki mashindano hayo zinatarajiwa kuamua mashindano hayo yafanyike wapi baada ya kumaliza kinyang'anyiro cha Shanghai huku kukiwa na taarifa maafisa wengi wanataka mashindano hayo yahamishiwe sehemu nyingine.

Taarifa hizi zinakuja wakati huu ambapo Uongozi wa Formula One hiyo jana ukiwa umetangaza hauna mpango wa kuyaondoa mashindano hayo huko Bahrain lakini kwa shinikizo hili chochote kinaweza kikatokea.

Bodi ambayo inasimamia mashindano hayo ya magari yaendayo kasi duniani maarufu kama Langalanga FIA tangu juma lililopita imekuwa ikifuatilia kwa karibu kile ambacho kinatokea nchini Bahrain.

Mapema madereva ambao wanashiriki mashindano ya mwaka huu Sebastian Vettel na Michael Schumacher walisema wapo tayari kushiriki mashindano yajayo ambayo yatafanyika huko Bahrain lakini kwa hali ilivyo haijabainika kama wataendelea na msimamo wao.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.