Pata taarifa kuu

Nguli wa Filamu Nchini Tanzania Steven Charles Kanumba azikwa na maelfu ya wananchi Dar Es Salaam

Msanii nguli wa Filamu nchini Tanzania ambaye alijikusanyia umaarufu wa kipekee katika Ukanda wa Maziwa Makuu na hata mataifa mengine ya Afrika, Ulaya na Marekani Steven Charles Kanumba amezikwa na maelfu ya wananchi ambao walitokeza kwenye safari yake hiyo ya mwisho.

Nguli wa Filamu Nchini Tanzania Steven Charles Kanumba enzi za uhai wake
Nguli wa Filamu Nchini Tanzania Steven Charles Kanumba enzi za uhai wake
Matangazo ya kibiashara

Kanumba ambaye alifariki usiku wa kuamkia jumamosi nyumbani kwake amezikwa katika Makuburi ya Kinondoni Jijini Dar Es Salaam ambapo maelfu ya mashabiki wake wa Filamu, Wasanii na hata Vionmgozi wa serikali walihudhuria shughuli hiyo ambayo inatajwa kuwa ni kihistoria.

Kanumba ambaye amejipatia umaarufu mkubwa kupitia sanaa ya uigizaji na filamu alikutwa na mauti akiwa na Mpenzi wake Elizabeth Michael ambaye ni muigizaji maarufu zaidi kwa jina la Lulu ambaye kwa sasa anashikiliwa kwa uchunguzi zaidi kubaini nini chanzo cha kifo cha msanii huyo.

Maelfu ya waombolezaji ambao walijitokeza kwenye mazishi hayo waliongozwa na Makamu wa Rais wa Tanzania Mohamed Ghalib Bilali pamoja na Mawaziri na Wabunge ambao walipata fursa ya kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa Marehemu Kanumba.

Simanzi kubwa ilitanda katika Jiji la Dar Es Salaam huku shughuli nuingi zikitatizika kutokana na wananchi wengi kujitokeza kwenye Viwanja wa Leaders Club kwa ajili ya kushuhudia shughuli za mazishi za Msanii huyo wa Filamu Steven Charles Kanumba.

Kwa sasa Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa kina kubaini chanzo cha kifo cha Kanumba huku pia wakiendelea kumhoji Elizabeth Michael lakini taarifa za awali za uchunguzi kama ambavyo zimetolewa na Kamanda wa Polisi Kanda ya Kinondoni ACP Charles Kenyela zinasema chumbani kwa marehemu kulikutwa pombe kali.

Steven Charles Kanumba Msanii nguli ambaye pia ni muasisi wa Filamu hapa nchini alizaliwa tarehe nane ya mwezi january mwaka elfu moja mia tisa themanini na nne na hadi anafikwa na umauti alikuwa ameshaigiza zaidi ya filamu arobaini na alikuwa mbioni kwenye Hollywood kwa kazi zake za kisanii.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.