Pata taarifa kuu
Malaysia

Langalanga: Lewis Hamilton ashinda mazoezi ya Malaysia Grand Prix

Bingwa wa dunia wa 2008 katika uendeshaji  magari aina ya langalanga au Formula One Lewis Hamilton,  raia wa Uingereza ameibuka mshindi katika majaribio ya mashindano ya Malaysia Grand Prix yanayomalizika Jumapili hii mjini Sepang.

Matangazo ya kibiashara

Dereva huyo wa magari ya McLaren alishinda majaribio ya asubuhi kwa muda wa dakika 1 sekunde 38 nukta 0 mbili ushindi ambao pia aliupata mchana kwa dakika 1 sekunde 38 nukta 1 saba.

Bingwa mara saba wa mashindano hayo Michael Schumacher, ambaye gari lake aina ya Mercedes limekuwa likiwavutia wengi kutokana na ubunifu wake aliibuka katika nafasi ya pili wakati Jenson Button ambaye pia yuko katika kundi la McLaren akimaliza katika nafasi ya tatu.

Bingwa wa mwaka jana,Sebastian Vettel wa kampuni ya magari ya  Red Bull alimaliza katika nafasi ya 10 kwa muda wa dakika 1 nukta 2 tatu.

Jenson Button wa Uingereza anaongoza msusururu wa mashindao hayo kwa alama 25,Sebastian Vettel wa Ujerumani ni wa pili kwa alama 18 wakati Lewis Hamiliton pia kutoka Uingereza akifunga tatu bora kwa alama 15.

Makala yajayo yatanadalia mjini Shanghai China mwezi wa Aprili kati ya tarehe 13 na 15.

Mashindano ya mwaka huu ya Formula one yana madereva 22 wanaowania ubingwa wa mwaka huu.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.