Pata taarifa kuu
Uganda

Mechi za ligi kuu ya soka nchini Uganda zimesimamishwa kwa muda kutokan a na mgomo wa wachezaji

Wachezaji wa Vilabu mbalimbali nchini humo chini ya muungano unaotetea maslahi yao FOFPA,wanasema wanataka maslahi yao kushughulikiwa,na pia wanataka kujiuzulu kwa viongozi wakuu wa shirikisho la soka nchini humo FUFA,kwa kile wanachodai kuwa wameshindwa kutekeleza majukumu yao.

Mwenyekiti wa ligi ya Soka nchini Uganda, Kavuma Kabenge
Mwenyekiti wa ligi ya Soka nchini Uganda, Kavuma Kabenge
Matangazo ya kibiashara

Mwenyekiti wa ligi hiyo ya soka,Kavuma Kabenge amesema wameafikiana na viongozi wa Vilabu vya soka nchini humo kusitisha Mechi zote zilizokuwa zimeratibiwa wiki hii ili wachezaji watatue matatizo yanayowakabili.

Miongoni mwa maswala nyeti yanayowakabili wachezaji wa Vilabu hivyo 16 ni pamoja na mfumo unaotumiwa kuwasajili wachezaji wapya.

Miongoni mwa mechi zilizosimamishwa ni Bidco dhidi ya Maroons na URA kucheza na Hoima-Busia. .

Mechi za ligi hiyo zinatarajiwa kurudiwa Jumanne juma lijalo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.