Pata taarifa kuu
FAINALI ZA KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA

Michezo 13 ya Kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2013 kupigwa hii leo

Michezo kumi na tatu ya kusaka tiketi ya kushiriki fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika za mwaka 2013 zinatakazoandaliwa nchini Afrika Kusini inatarajiwa kupigwa hii leo jumatano ambao michezo ya marudiano itashuhudiwa ikipigwa juma la pili la mwezi Juni.

Uwanja wa Soccer City unaotarajiwa kutumika kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2013
Uwanja wa Soccer City unaotarajiwa kutumika kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2013
Matangazo ya kibiashara

Tanzania maarufu kama Taifa Stars itakuwa mwenyeji wa Msumbiji inayojulikana kama Mambas mchezo ambao utapigwa kwenye Dimba la Taifa ambapo Kocha Mkuu Jan Poulsen amejigamba kuondoka na ushindi.

Licha ya Taifa Stars kutokuwa na rekodi nzuri mbele ya Msumbiji timu hiyo imejiapiza kuhakikisha inapata ushindi kwenye mchezo huo kabla ya kurejea mnamo mwezi June mwaka huu.

Kenya maarufu kama Harambee Stars wao watakuwa na kibarua mbele ya Togo wakati huu ambapo mshambuliaji wao McDonald Mariga akijiondoa kwenye Kambi kutokana na kuibuka kutokelewana baina yake na Chama Cha Soka nchini humo.

Rwanda inayotambulika kwa jina la Amavubi yenyewe itakabiliana na Nigeria wanaojulikana kwa jina la Super Eagles wakati Burundi inayojulikana kwa jina la Utani la Inamba Murugamba yenye itakuwa inatoana jasho na Zimbabwe.

Jamhuri ya Kidemokasia ya Kongo DRC maarufu kama Leopards yenyewe itapimana ubavu na Ushelisheli wakati Simba wasiofugika Cameroon wao watakuwa uwanjani kupepetana na Guinea Bissau.

Ethiopia wao watacheza na Benin wakati mchezo mwingine utashuhudia Uganda wakicheza na Congo Brazzaville huku Gambia wakiwa wenyeji wa Algeria wakati Malawi watakuwa na shughuli pevu mbele ya Chad.

Michezo mingine itawakutanisha Madagascar wataocheza na Cap Verde huku Liberia wakitoshana nguvu na Namibia huku Sao Tome wakikabiliana uso kwa uso Sierra Leone.

Mchezo kati ya Misri na Jamhuri ya Afrika Ya Kati umesogezwa mbele kutokana na hali ya usalama huko Cairo ikionekana kutetereka.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.