FA kumtaja Mrithi wa Fabio Capello
Shirikisho la soka nchini Uingereza, limeanza Mchakato wa kuanza kumpata Kocha mpya wa timu ya Taifa ya Uingereza baada ya Fabio Capello kujiuzulu wadhifa huo kufuatia sakata la John Terry.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Kumekuwa na tetesi kuwa huenda Kocha wa tottenham hotspur, Harry Redknapp akamrithi Capello aliyejiuzulu usiku wa jana baada ya kuukosoa hadharani uamuzi FA kumvua unahodha Mchezaji wa Chelsea, John Terry.
Uamuzi wa Capello wa kushtukiza umefanyika wakati ambapo pia Kocha wa Tottenham kukutwa hana hatia na mahakama ya Southwark alipokuwa akikabiliwa na shutma za kukwepa kulipa Kodi.
FA itafanya mkutano na waandishi wa Habari hii leo ili kumteua mrithi kabla ya Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya, michuano itakayopigwa Miezi minne ijayo.