Pata taarifa kuu
EQUATORIAL GUINEA-GABON

Angola na Cote D'Ivoire wapata ushindi kwenye michezo yao ya awali Kombe la Mataifa ya Afrika

Timu ya Taifa ya Angola imeanza vizuri mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika yanayofanyika nchini Equatorial Guinea na Gabon kwa kupata ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Burkina Faso.

Matangazo ya kibiashara

Mchezo huo kutoka Kundi B ulipigwa kwenye Uwanja wa Malabo na kushuhudia vijana wa Angola wakionesha uchu wao wa kutaka ushindi na kufanikiwa kuibuka na pointi tatu muhimu.

Goli la Mshambuliaji wa zamani wa Manachester United Mateus Alberto Contreiras Gonçalves maarufu kama Manucho lilitosha kupeleka furaha nchini Angola na kuwafanya wawe vinara wa Kundi B.

Angola walikuwa wa kwanza kupata goli kupitia kwa Mateus lakini Alain Traore alisawazisha goli hilo kupitia faulo aliyoipiga umbali wa mita ishirini na tano na kujaa wavuni na kumshinda Kipa wa timu hiyo.

Kocha wa Angola Paulo Duarte baada ya mchezo huo alisema ushindi huo umechangiwa kwa kiasi kikubwa na kujitoma kwa wachezaji wake ambao walipambana kwa kiwango kikubwa na kuibuika washindi.

Mchezo wa mapema ulishuhudia Cote D'Ivoire ikipata ushindi mwembamba wa goli moja kwa nunge mbele ya Sudan ambayo licha ya kukosa wachezaji wa kulipwa walifanikiwa kupambana kwa kiwango kikubwa.

Tembo hao walifanikiwa kupata goli lao kupitia Mshambuliaji wake anayekipiga katika Klabu ya Chelsea Didier Drogba na hivyo kushika nafasi ya pili kwenye Kundi B.

Baada ya mchezo huo Nahodha wa Cote D'Ivoire Drogba amesema ushindi ulikuwa ni muhimu sana na sasa wanajipanga na mchezo wao dhidi ya Burkina Faso wakati Angola watakuwa na kibarua dhidi ya Angola.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.