Pata taarifa kuu
UINGEREZA

Beckham kujiunga tena na LA Galaxy

Nahodha wa zamani wa timu ya England David Bechkham anarejea katika timu ya Los Angeles Galaxy kwa mkataba wa miaka miwili.

Nyota wa mpira wa miguu David Beckham
Nyota wa mpira wa miguu David Beckham REUTERS/Brandon Malone
Matangazo ya kibiashara

Beckham amesema kuwa uamuzi wake wa kurejea katika timu hiyo ni muhimu kwake kutokana na kwamba amepata maombi kutoka kwa klabu mbalimbali duniani,ingawa bado anapenda kucheza Marekani.

Beckham alimaliza mkataba wake wa miaka mitano na klabu ya Galaxy mwaka uliopita na kumekuwepo na fununu zilizoenea kuwa Beckham amekuwa akifikiria kukubali maombi ya klabu ya Paris St. Germain na baadhi ya klabu za Uingereza.

Hata hivyo mapema mwezi huu klabu hiyo ilisema kuwa Beckham hatajiunga tena na timu hiyo kutokana na sababu za kifamilia.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.