Pata taarifa kuu
CECAFA-TANZANIA

Rais wa CECAFA Leodegar Tenga afanikiwa kutetea nafasi yake

Mashindano ya kombe la Challenge kwa nchi za Afrika Mashariki yanayosimamiwa na Baraza la Vyama vya Soka vya Afrika Mashariki CECAFA, yaanza kutimua vumbi hii leo jijini Dar es Salaam Tanzania.

Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania ambao ni mabingwa watetezi wa kombe la Chalenji (CECAFA)
Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania ambao ni mabingwa watetezi wa kombe la Chalenji (CECAFA) Online
Matangazo ya kibiashara

Mechi hizo ambazo zote zitapigwa katika dimba la uwanja wa Taifa, itashuhudiwa mechi za ufunguzi za awali ambapo timu ya Taifa ya Burundi itapambana na Timu ya Taifa ya Somalia katika mchezo utakaoanza maajira ya sanane mchana kwa saa za Afrika Mashariki.

Mchezo mwingine utakaofuata baada ya ule wa awali uzikutanisha timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) ambao watacheza na timu ya Taifa ya Uganda (Uganda Cranes) katika mchezo ambao unatabiriwa kuwa mgumu na wakuvutia kutokana na aina ya mchezo ambao timu hizo zinacheza, mchezo huo utaanza maajira ya sakumi jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Wakati michuano hiyo ikianza, hapo jana CECAFA ilikuwa inafanya uchaguzi wake mkuu jijini Dar es Salaam ambapo imeshuhudiwa rais wa sasa wa chama hicho Leodegar Chila Tenga akifanikiwa kutetea nafasi yake baada ya kupata kura 11 na hii nikutokana na kutofika kabisa kwa mpinzani wake Eadoul Husein wa Djibouti.

Akitangaza matokeo hayo, katibu mkuu wa CECAFA Nicholas Musonye amesema kuwa ushindi huo wa Tenga ni Ishara tosha kuwa wanachama wa CECAFA bado wana imani na uongozi wake na kutokana na mabadiliko ambayo ameyaleta.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.