Pata taarifa kuu
UJERUMANI

Japan na Marekani kucheza fainali ya kombe la dunia la wanawake

Mashindano ya kombe la dunia kwa upande wa wanawake yanayoendelea nchini Ujerumani, yameendelea kushika kasi ambapo sasa yametinga katika hatua ya fainali itakaoshuhudiwa ikipigwa siku ya jumapili kati ya Marekani na Japan.

Wachezaji wa timu ya taifa ya Japan wakishangilia moja ya magoli waliyofunga
Wachezaji wa timu ya taifa ya Japan wakishangilia moja ya magoli waliyofunga Online
Matangazo ya kibiashara

Katika mechi za nusu fainali zilizochezwa hiyo jana, timu ya taifa ya wanawake ya Japan ilifanikiwa kutinga katika hatua ya fainali baada ya kufanikiwa kuchomoza na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya timu ya taifa ya Sweeden.

Mchezo huo ambao ulishuhudia Sweeden wakiwa wa kwanza kuzifumania nyavu za Japan kabla ya Japan kuja juu na kufanikiwa kurejesha goli hilo na kuongeza mengine mawili.

Mchezo mwingine wa nusu fainali uliwakutanisha timu ya taifa ya Marekani ambao walikuwa na kibarua dhidi ya timu ya taifa ya Ufaransa na kushuhudia timu ya wanawake ya Marekani ikifuzu hatua ya fainali kwa kuichapa Ufaransa kwa mabao 3-1.

Nchi ya Marekani inacheza fainali za tatu za mashindano hayo baada ya kufanikiwa kutwaa taji hilo mwaka 1991 na 1999 huku nchi ya Japan ikiwania kutwaa taji hilo kwa mara ya kwanza.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.