Pata taarifa kuu

Mashindano ya Kagame Cup yaingia robo fainali, Novak Jokovich amshinda Rapahel Nadal

Michuano ya klabu bingwa Afrika mashariki na kati maarufu kama Kagame cup inayoendelea nchini Tanzania, imeendelea kushika kasi ambapo sasa mashindano hayo yametinga katika hatua ya robo fainali. 

Matangazo ya kibiashara

Katika mechi zilizochezwa jana jioni, timu ya soka ya Ocean View kutoka zanzibar ilijikuta ikiaga mashindano hayo baada ya kuanza vizuri mechi zake za awali na jana kujikuta wakifungwa kwa bao 1-0 dhidi ya klabu ya Vital'o Football Club kutoka Burundi.

Mchezo mwingine ulikuwa ni kati ya simba ya Tanzania waliocheza na Red Sea na kushuhudia mchezo huo ukimalizika kwa sare ya bila kufungana.

Mpaka sasa timu zilizofuzu hatua ya robo faina itakayoanza kesho Jumanne ni pamoja na Simba na Yanga za Tanzania, ulinzi ya Kenya, St. George ya Ethiopia, Red Sea, Bunamwaya ya Uganda, Vital'o ya Burundi na El Mereikh ya Sudan.

Nchini Uturuki, polisi imewakamata wachezaji na maofisa kadhaa wa mpira nchini humo kwa tuhuma za kupanga matokeo, ambapo inamshikilia rais wa klabu ya Fenarbache, Aziz Yildirim kwa tuhuma za kuhusika na timu yake kupanga matokeo ili kutwaa ubingwa wa nchi hiyo.

Zaidi ya watu 40 wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma hizo.

TENNESI.

Katika mashindano ya tennesi ya Wimbledon mchezaji Novak Jokovich amefanikiwa kutwaa taji la michuano hiyo baada ya kumfunga bingwa nambari moja wa mchezo huo Rafael Nadal katika mchezo ulioshuhudiwa na maelfu ya mashabiki wa mchezo huo.

NGUMI.

Kufuatia kushindwa pambano lake ya uzito wa juu siku ya Jumapili na mpinzani wake Wladimil Klitschko bondia toka uingereza David Haye ameapa kuomba mpambano wa marudiano na mpinzani wake.

Katika mchezo huo uliofanyika siku ya jumamozi kuamkia jumapili majaji wa mchezo huo walimpa ushindi wa pointi bondia Klitschko na kumaliza ubishi uliokuwepo kati ya mabondia hao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.