Pata taarifa kuu
Uingereza

Wimbledon: Roger Federer ataraji kurejea kileleni

michuano ya Tenesi ya Wimbledon nchini Uingereza imepangwa kuzinduliwa Jumatatu Juni 20 na kutamatishwa Julay 3 mwaka huu. Kwa wavulana anategemewa kati ya Rafael Nadal, Novak Djokovic, Roger Federer et Andy Murray.Ikiwa Rafa na Djoko wapo katik ahali nzuri katika kipindi cha mwaka mzima, Federer yupo katika wakati mzuri mzuri ya kushinda taji yake ya saba katika michuano hiyo inayo fanyika jijini London. 

Uwanja wa Wimbledon Ukifunikiwa kwa kuzuia mvua
Uwanja wa Wimbledon Ukifunikiwa kwa kuzuia mvua EUTERS/Toby Melville
Matangazo ya kibiashara

Wachezaji bingwa 4 duniani wa mchezo huo ndio waliowika wakati wa upigaji kura siku ya Ijumaa iliopita. Hata hivyo kumeonekana kuibuka kwa vipaji vipya kama vile namba 46 na namba 99 kwenye orodha ya ATP ikiwa ni pamoja na mmarekani John Isner na mfaransa Nicolas Mahut. Mwaka jana katika uwanja wa mashindano wachezaji hao 2 walichuana katika maechi ya kwanza ndevu katik ahistoria ya chezo huo wa Tenesi kwa masaa 11h05 (6-4, 3-6, 6-7, 7-6, 70-68 kwa faida ya Isner) ni kwa bahati nasibu tena wakutana wachezaji hao ili kuuunda mzunguuko huo wa kwanza.

Baada ya mzunguuko huo wa kwanza kumalizika, watazamaji watakodolea macho zaidi, mchuano baina ya bingwa wa dunia Rafael Nadal bingwa mwaka (2008 na 2010) ambae pia alitwaa kombe la Roland Garros, taji la la kumi ambae atapamabana na Djokovic.

Upande wake Andy Murray amepuuza uwezekano wa kucheza na mchezaji bora zaidi duniani, Rafael Nadal, katika nusu fainali ya Wimbledon, akisema muhimu kwanza ni kuangazia pambano lake la raundi ya kwanza.

Murray, ambaye amepangwa katika mapambano hayo kucheza dhidi ya Nadal katika wachezaji wanne wa mwisho watakaosalia, amesema muhimu zaidi hivi sasa ni kufikiria namna atamshinda Daniel Gimeno-Traver kutoka Uhispani katika raundi ya kwanza.

Baada ya Roger Federer kutolewa jasho na Alejandro Falla mwaka jana katika raundi ya kwanza, Murray, mwenye umri wa miaka 24, kamwe hataki kufanya mzaha katika mashindano hayo.

Federer mwaka jana alihitaji kucheza seti tano ili kumshinda Falla, na Murray hana matazamio ya mchezo rahisi dhidi ya Gimeno-Traver, ambaye katika orodha ya wachezaji bora ulimwenguni, amepangwa katika nafasi ya 56.

Mchezaji huyo wa Uskochi aliibuka bingwa katika mashindano ya Uingereza ya Queen's Jumatatu iliyopita, lakini ataingia pambano la Wimbledon akihisi kana kwamba amepungukiwa kwa kutofanya mazoezi ya kutosha, baada ya mvua kutatiza pambano la kuonyesha uhodari wake dhidi ya Viktor Troicki, kutoka Serbia, kukatizwa kwa mvua siku ya Ijumaa.

Alikuwa akiongoza 4-1 wakati pambano hilo la Boodles Challenge, katika uwanja wa Stoke Park, Buckinghamshire, kusimamishwa.

Katika mashindano ya Wimbledon, Andy Murray amepangwa katika nafasi ya nne, baada ya Nadal, Djokovic na Federer.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.