Pata taarifa kuu
FORMULA ONE-BAHRAIN

Bernie Ecclestone: Bado hatuna uhakika kama mashindano ya Bahrain Grand Prix yatafanyika kama yalivyopangwa

Rais wa chama magari yaendayo kasi zaidi duniani ya Formula Bernie Ecclestone ametangaza kurejesha mashindani ya Bahrain Grand Prix kwenye kalenda ya chama hicho lakini akisistiza yanaweza yasifanyike.

Uwanja uliokuwa yafanyike mashindano ya F1 wa nchini Bahrain ukilindwa na Polisi: March mwaka huu
Uwanja uliokuwa yafanyike mashindano ya F1 wa nchini Bahrain ukilindwa na Polisi: March mwaka huu REUTERS/Caren Firouz
Matangazo ya kibiashara

Rais huyo amesema kuwa mara baada ya kamati ya utendaji ya FIA kukutana wameamua kuyarejesha katika ratiba mashindano yaliyotakiwa kufanyika nchini Bahrain mwezi wa tatu mwaka huu na sasa yatafanyika mwezi wa October ingawa bado haijawekwa wazi rasmi kama kweli yatafanyika.

Mashindano ya bahrain Grand Prix yaliahirishwa kufanyika mwezi March mwaka huu nchini humo kutokana na machafuko yaliyokuwa yakiendelea na kusababisha kushindwa kufanyika kwasababu za kiusalama.

Hata hivyo bosi huyo amesema kuwa kulikuwa na mvutano mkubwa kati ya wajumbe wakati wakuamua kuyarejesha katika ratiba mashindano hayo ambapo hawajakubalina kamayafanyike nchini humo kama yalivyopangwa badala yake kutategemea hali ya usalama itakavyokuwa wakati huo.

Upinzani wakati wa kujadili swala la Bahrain uliibuka pale wawakilishi wa timu 12 ambazo zinashiriki mashindano hayo kukataa kushiriki katika mbio za Bahrain wakisema hali ya usalama bado itakuwa haijatengamaa.

Kurejeshwa katika kalenda kwa mashindano ya Bahrain kumekuja kufuatia mashindano yaliyotakiwa kufanyika nchini India tarehe 30 cotober lkusogezwa mbele hadi december 11.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.