Man United kucheza fainali na Barcelona
Timu zitakazokutana fainali ya klubu bingwa barani Ulaya sasa zimejulikana. Manchester United ya Uingereza itakutana na Barcelona ya Uispania.
Imechapishwa:
Manchester United itakutana na Barcelona kwenye fainali ya klabu Bingwa Ulaya baada ya kuicharaza Schalke 04 ya Ujerumani kwa magoli 4-1.
Magoli ya Manchester United yalifungwa na Antonio Valencia, Darron Gibson, na Anderson akufunga magoli mawili.
Katika mchezo wa kwanza Man United ilipata ushindi wa mabao 2-0.
Barcelona iliingia fainali baada ya kuifunga Real Madrid 3-1 baada ya michezo miwili ya nusu fainali.
Fainali ya Klabu Bingwa Ulaya itachezwa kwenye uwanja wa Wembley, tarehe 28 mwezi Mei.