Pata taarifa kuu
ISRAEL-PALESTINA-USALAMA

Ghasia mpya zazuka kati ya Waisrael na Wapalestina

Vurugu mpya zimeibuka Ijumaa wiki hii katika Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi, ambapo vijana wawili wa Israel wamejeruhiwa na risasi, na kusababisha kuongezeka kwa mvutano unaoendelea kabla ya ziara ya Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu mjini Washington.

Mmoja wa vijana wawili waliojeruhiwa katika mji wa Hebroni akiwasili katika hospitali ya Shaare Zedek ya Jerusalem, Novemba 6, 2015.
Mmoja wa vijana wawili waliojeruhiwa katika mji wa Hebroni akiwasili katika hospitali ya Shaare Zedek ya Jerusalem, Novemba 6, 2015. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika mji wa Hebroni, karibu na makaburi ya watu wa zamani, eneo patakatifu kwa Wayahudi na Waislamu linalosababisha mvutano, Waisrael wawili wenye umri wa miaka 16 na 18 wamejeruhiwa na watu wenye silaha wasiojulikana, jeshi limebaini.

Katika sekta hiyo ya Hebroni, Mpalestina mwenye umri wa miaka 72 amepigwa risasi na jeshi la Israel, ambalo linamshutumu kuendesha shambulizi kwa kutumia gari. "Wanajeshi waltambuliwa tishio na wakajibu kwa kumfyatulia risasi mshambuliaji ", msemaji wa kijeshi ameliambia shirika la habri la Ufaransa la AFP.

Kwa mujibu wa hospitali ya Israel ambako alipelekwa, mwanamke huyo alikuwa amekwisha kufa.

Vyanzo vya kimatibabu vya Palestina vimemtambua mwanamke huyo kama Tharwat Chaaraoui na kubaini kwamba alikuwa akiendesha gari katika mvua kubwa wakati huo, na kuthibitisha kwamba hakuwa na nia yoyote ya kuwashambulia wanajeshi.

Ijumaa wiki hii, pia katika Ukingo wa Magharibi, Mpalestina mmoja amemjeruhi vikali kwa kisu Muisrael mbele ya jengo la kibiashara katika eneo la Shaar Binyamin linalokaliwa na walowezi, kabla ya kutoweka, kwa mujibu wa jeshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.