Pata taarifa kuu
UN-PALESTINA-ISRAEL-USALAMA-DIPLOMASIA

Ban Ki-moon atoa wito kwa Israel na Palestina kurejesha hali ya utulivu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ambaye anazuru Israel na Palestina ametoa wito wa kusitishwa kwa makabiliano yanayoendelea kushudiwa kati ya Waisraeli na Wapalestina.

Katibu Mkuu wa UN, Ban Ki-moon na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu katika mkutano na wanahabari wa habari, Oktoba 20, 2015 Jerusalem.
Katibu Mkuu wa UN, Ban Ki-moon na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu katika mkutano na wanahabari wa habari, Oktoba 20, 2015 Jerusalem. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika siku ya pili ya ziara yake ya kushitukiza Mashariki ya Kati kwa kujaribu kutuliza mvutano kati ya Israel na Palestina, Ban pia atalielezea Baraza la Usalama, kupitia kupitia teknolojia ya kisasa, maendeleo ya mazungumzo kati ya pande hizo mbili. Ni kwa ombi la Katibu Mkuu ambapo mkutano huo umeitishwa kwa "dharura", kuanzia saa 9:00 alaasiri saa za Mashariki ya Kati (sawa na 1:00 usiku saa za kimataifa), wanadiplomasia wamesema Jumanne wiki hii mjini New York.

Akizungumza akiwa mjini Jerusalem, Ban Ki-moon ameonya kuwa hatua za dharura zinastahili kuchukuliwa kuzuia machafuko hayo kusambaa zaidi na kugeuka kuwa ya kidini.

Naye Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amekanusha tuhma za nchi yake kutumia nguvu kupita kiasi kudhibiti makabiliano hayo na kusisitiza kuwa kama taifa inajilinda.

Kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa raia wa Palestina na Israel wamekuwa wakishambuliana na hadi sasa Wapalestina 50 na Waisraeli 9 wameuawa kwa kudungwa visu na kupigwa risasi Mashariki mwa mji wa Jerusalem na Ukingo wa Magharibi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.