Pata taarifa kuu
ISRAELI-PALESTINA-USALAMA

Mashambulizi mapya dhidi ya Israel karibu na mji wa Hebron

Mji wa Hebron, Kusini mwa Ukingo wa Magharibi, umeshuhudia machafuko Jumapili hii, ikiwa ni pamoja na shambulizi la kisu na shambulizi lingine kwa gari dhidi ya wanajeshi na askari polisi wa Israel, jeshi na polisi vimebaini.

Vikosi vya usalam vya Israel na maafisa wa Idara za huduma za dharura katika eneo la shambulizi la garidhidi ya askari polisi walinzi wa mpaka wa Israel katika mji wa Beit Hanoun, kaskazini mwa Hebron, Novemba 1, 2015.
Vikosi vya usalam vya Israel na maafisa wa Idara za huduma za dharura katika eneo la shambulizi la garidhidi ya askari polisi walinzi wa mpaka wa Israel katika mji wa Beit Hanoun, kaskazini mwa Hebron, Novemba 1, 2015. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Mshabuliaji wa kisu, raia wa Palestina, ameuawa na wanajeshi wa Israel, jeshi limearifu. Mshambuliaji mwengine aliyetumia gari alitimka baada ya kuwajeruhi askari polisi watatu, polisi imebaini.

Matukio hayo yametokea karibu na mji wa Beit Hanoun, si mbali na makazi ya Wayahudi ya Qiryat ambako kunashuhudiwa vuruguza kila mara.

Mapema Jumapili mchana , " raia mmoja wa Palestina amejaribu kumchoma kisu askari wakati wa makabiliano ya vurugu katika mji wa Beit Hanoun. Wanajeshi waliotumwa eneo hilo wamejibu haraka kwa tishio hilo kwa kumuua kwa risasi mchambuliaji " , jeshi la Israel limesema katika taarifa yake.

Mshambulizi ametambuliwa na vyanzo vya hospitali vya Palestina kama Feroukh Fadi, mwenye umri wa miaka 27.

Baadaye, askari watatu walinzi wa mipaka wa Israel wamejeruhiwa karibu na mji wa Beit Hanoun katika shambulizi la gari, polisi ya Israel imebaini.

Afisa mmoja anasumbuliwa na majeraha makubwa na wengine wawili wamepata majeraha madogo, kwa mujibu wa Idara ya huduma za dharura za Israel. askari polisi katika eneo la tukio walirusha risasi lakini muhusika wa shambulizi alitimka, polisi imesema.

Eneo zima la Hebron linakabiliwa na mvutano kati ya Wapalestina na walowezi wa Kiyahudi, ambao wanaishi chini ya ulinzi wa majeshi ya Israel.

Tangu Oktoba 1, vurugu hizo zilmesababisha vifo vya watu kati ya Wapalestina, ikiwa ni pamoja na Waarabu wa Kiisrael, na tisa mongoni mwa Waisrael. Nusu ya Wapalestina waliuawa walitenda kutenda au kujaribu kufanya mashambulizi, hasa kwa kisu dhidi ya wanajeshi, askari polisi au raia wa Israel.

Mashambulizi yalianza katika mji mkongwe wa Jerusalem, ambapo kunapatikana Msikiti mtakatifu kwa Waislam wa Al Aqsa, lakini mashambulizi hayo kwa sasa ymeendelea kushuhudiwa katika mji wa Hebron.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.