Pata taarifa kuu
KENYA-UGAIDI-HAKI

Kenya: Washirika wawili katika shambulio la Westgate wahukuhumiwa kifungo cha miaka 18

Mahakama ya Kenya imewahukumu leo Ijumaa washirika wawili katika shambulio la Westgate kifungo cha miaka 18 jela baada ya kupatikana na hatia mwanzoni mwa mwezi Oktoba.

Mtu huyu akisoma gazeti ambalo limechapisha picha za wahanga wa shambulio dhidi ya jumba la kibiashara la Westgate, Nairobi Kenya.
Mtu huyu akisoma gazeti ambalo limechapisha picha za wahanga wa shambulio dhidi ya jumba la kibiashara la Westgate, Nairobi Kenya. AFP PHOTO / SIMON MAINA
Matangazo ya kibiashara

Wawili hao wanashtumiwa "kula njama" kwa vitendo vya kigaidi na "kuunga mkono" kundi la magaidi waliotekeleza shambulio dhidi ya jumba la kibiashara cha Westgate jijini Nairobi mnamo mwaka wa 2013, kulingana na shirika la habari la AFP.

Washukiwa hao Mohamed Ahmed Abdi na mwenzake Adan Hussein Mustafa wanadaiwa kushirikiana kutekeleza ugaidi pamoja na kusaidia wakati wa shambulizi hilo. Mshukiwa mmoja liban abdullahi hata hivyo aliachiliwa huru kwa kukosa ushahidi wa kutosha.

Mshukiwa wa nne Adan Dheq aliachiliwa huru Januari 2019 baada ya mahakama kushindwa kupata ushahidi wa kutosha dhidi yake.

Shambulio la Westgate lilitokea mwaka wa 2013 ambapo watu 67 walipoteza maisha yao na wengi kuachwa na majeraha mabaya.

Kundi la kigaida la al- Shabaab lilikubali kutekeleza shambulio hilo kupitia vyombo vya habari.

Watu zaidi ya 20 walikwama kwenye jumba hilo, baadhi walinusuriwa lakini wengine akiwemo afisa wa polisi na raia wa kigeni walipoteza maisha yao.

Hata hivyo, magaidi watano waliuawa na maafisa wa polisi waliofika eneo hilo kuwanusuru zaidi ya watu 600 waliokuwa walikwama kwenye jengo hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.