Pata taarifa kuu
KENYA-CORONA-AFYA

Rashid Aman: Kenya haipo tayari kwa wimbi lingine la COVID-19

Wizara ya afya nchini Kenya imeonya kuwa huenda serikali ikarudi kufunga shule kwa mara nyingine ,iwapo nchi hiyo itaendelea kushuhudia ongezeko la kasi kwa maambukizi ya virusi vya Corona.

Maafisa wa afya wakishughulikia mgonjwa na COVID-19, huko Machakos (Kenya), Agosti 3, 2020.
Maafisa wa afya wakishughulikia mgonjwa na COVID-19, huko Machakos (Kenya), Agosti 3, 2020. TONY KARUMBA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hii ni baada ya jumla ya maambukizi nchini humo kufikia elfu 41 mia tisa na thelathini saba , maambukizi mapya ya kila siku yakiwa zaidi ya mia tatu katika siku kadhaa zilizopita.

Hata hivyo Katibu mkuu katika wizara ya afya Rashid Aman amesema kuwa Kenya haipo tayari kwa wimbi lingine la COVID-19.

Mlipuko wa virusi vya corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa COVID-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.