Pata taarifa kuu
KENYA-USALAMA

Jeshi la Kenya laendelea kupata umaarufu barani Afrika

Wakati Kenya ikiadhimisha siku ya wanajeshi,jeshi la Kenya Defence Forces  bado linaendelea kuwa na umaarufu wake katika Bara la Afrika kutokana na mafunzo na ushirikiano na nchi kama Israel, Marekani na Uingereza.

Jeshi la Kenya linaendelea kukabiliana na mashambulizi mbalimbali nchini Somalia na Kenya.
Jeshi la Kenya linaendelea kukabiliana na mashambulizi mbalimbali nchini Somalia na Kenya. RFI/Stéphanie Braquehais
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo Tishio kubwa linaloendelea kuyakabili majeshi ya ukanda huu ni kundi la kigaidi la Al shabab ambalo limesababisha maelfu ya watu kupoteza maisha na wengine kulazimika kutoroka jeshini.

Jeshi la Kenya linaendelea kukabiliana na mashambulizi mbalimbali nchini Somalia na Kenya.

Tarehe 14 Oktoba ikiwa ni siku ya wanajeshi wa Kenya maarufu kama 'KDF day', rais Uhuru Kenyatta alihudhuria sherehe hizo katika kambi ya kijeshi ya Lanet huko Nakuru.

Rais Kenyatta alitumia fursa hiyo kuwakumbuka wanajeshi walioaga katika vita dhidi ya kundi la Al Shabab nchini Somalia. Hii ilikuwa mara ya pili pia kwa rais Kenyatta kuvaa magwanda rasmi ya jeshi.

Wanajeshi wa Kenya na jamaa zao wameshiriki sherehe maalum kuadhimisha siku ya idara ya jeshi la Kenya KDF.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.