Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Kamala Harris: Rais wa Tanzania ni 'bingwa' wa demokrasia

Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris Alhamisi mjini Dar es Salaam alimtaja Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kama 'bingwa' wa demokrasia katika awamu ya pili kati ya tatu ya ziara yake barani Afrika.

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwapungia wananchi wake. Tarahe 20 03 2023
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwapungia wananchi wake. Tarahe 20 03 2023 © IkuluTanzania
Matangazo ya kibiashara

Bi. Harris, mwanamke wa kwanza na mtu wa kwanza wa rangi kuchaguliwa kuwa makamu wa rais wa Marekani, amezungumza pamoja na Bi Hassan, ambaye Machi 2021 alikua mwanamke wa kwanza kuiongoza Tanzania. Samia Suluhu Hassan amemrithi akiwa kama Makamu rais John Pombe Magufuli aliyefariki dunia ghafla. Hivi majuzi alijitahidi kuachana na urithi wa kimabavu wa Magufuli na kuongeza dalili za uwazi.

Makamu wa rais wa Marekani amebaini kwamba wakati wa ziara yake katika nchi hii ya Afrika Mashariki, atajadiliana na Bi. Hassan, akimwita "bingwa", kuhusu demokrasia, utawala bora, ukuaji wa uchumi wa muda mrefu na mgogoro wa Tabia nchi. "Katika suala la ukuaji wa uchumi, utawala bora unatoa utabiri, utulivu na sheria ambazo biashara zinahitaji kuwekeza," Harris amesema.

"Kuna uwezekano wa kukua hapa," ameongeza. Bi Harris pia ameweka shada la maua katika kumbukumbu ya shambulizi dhidi ya ubalozi wa Marekani jijini Dar es Salaam, mji mkuu wa kiuchumi wa nchi hiyo, ulioshambuliwa mwaka 1998 kwa wakati mmoja na ubaloz w Marekani nchini Kenya, Nairobi.

Mashambulizi haya mawili yaliyotokea karibu kwa wakati mmoja, yaliyodaiwa na Al-Qaeda, yalisababisha vifo vya zaidi ya watu 200 na wengine 5,000 kujeruhiwa. Ziara ya Bi Harris, iliyofuatana katika nchi za Ghana, Tanzania na Zambia, ni sehemu ya juhudi za Washington kuimarisha uhusiano wake na bara hilo ili kukabiliana na ushawishi wa China na Urusi.

Bi Hassan, ambaye alisherehekea mwaka wa pili tangu aingie madarakani Machi 19, alikuwa ameibua matumaini baada ya utawala wa Magufuli uliosababisha washirika kadhaa wa kimataifa kuipa kisogo Tanzania. Tanzania ilifanya uchaguzi wake wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1995, tangu wakati huo Chama Cha Mapinduzi (CCM) cha Bi. Suluhu wakati huo chama kimoja kilishinda chaguzi zote .

Mwezi Januari, alitangaza kufuta zuio la Mheshimiwa Magufuli la mikutano ya kisiasa na kufungua njia ya kurejea nchini kwa viongozi wa upinzani kama vile Tundu Lissu na Godbless Lema, uhamishoni kwa miaka mitano na miaka miwili mtawalia. Mwanzoni mwa mwezi Machi, alikuwa ameahidi kuzindua upya mchakato wa marekebisho ya katiba, madai ya zamani ya upinzani.

Siku ya Jumatano mjini Accra, makamu wa rais wa Marekani alitangaza mpango wa zaidi ya dola bilioni 1 kwa ajili ya kuwakomboa kiuchumi wanawake katika bara hilo. Katika hotuba yake, alibainisha maeneo matatu ambayo Washington inadhani yanaweza kufaidika kutokana na uwekezaji zaidi: uwezeshaji wa wanawake, uchumi wa kidijitali, na utawala bora na demokrasia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.