Pata taarifa kuu

Ukraine: Mapigano yaendelea kurindima licha ya makubaliano ya usitishwaji vita

Kulingana na ripoti ya Umoja wa mataifa, kwa uchache watu 331 wamelifariki tangu yalipoafikiwa makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya waasi na serikali, mashariki mwa Ukraine.

Basi liliyoshambuliwa kwa roketi Donetsk, jumatano Septemba 1 mwaka 2014.
Basi liliyoshambuliwa kwa roketi Donetsk, jumatano Septemba 1 mwaka 2014. REUTERS/Shamil Zhumatov
Matangazo ya kibiashara

Kwa jumla mapigano yaliyotokea katika eneo la DonBass yalisababisha vifo vya watu 3600 na wengine 9000 walijeruhiwa.

Ni vigumu kupata idadi kamili ya watu waliofariki au kujeruhiwa katika mapigano nchini Ukraine. Ripoti hiyo imebaini kwamba huenda idadi hiyo ikazidi.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa watu yumkini 10 wanafariki kwa siku katika eneo la Donbass, huku milipuko ya mabomu na milio ya risase vikiendelea kusikika katikati ya mji mkuu wa waasi Donetsk, na hali hiyo haimshangazi mtu yeyote.

Hayo yakijiri, watu 8 waliuawa jumatano wiki hii na wengine tisa kujeruhiwa katika mlipuko wa bomu liliyorushwa katika eneo la kibiashara mjini Donbass.

Katika mkutano na waandishi wa habari, Waziri mkuu wa eneo liliyojitenga la Donetsk, Alexander Zakharchenko, amesema hajui kinachoendelea kuhusu makubalinao hayo ya usitishwaji mapigano.

“ Sijui kinachoendelea kuhusu makubaliano hayo, kwani watu wanaendelea kuuawa, huku mapigano yakiripotiwa katika baadhi ya maeneo, kwa hiyo ni ubora tu nichukuwe bunduki yangu na kuelekea kwenye uwanja wa ndege nianzishe mapigano”, amesema Zakharchenko.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.