Pata taarifa kuu
Soka Barani Afrika-AFCON 2015

Cote d'Ivoire na Guinea zatoka sare

Pamoja na sare ya kufungana bao1-1 kati ya Cote d'Ivoire na Guinea katika duru ya kwanza ya michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika AFCON 2015, timu zote mbili zilionekana kuridhishwa na alama zilizopata, katika mchuno uliyopigwa Jumanne Januarri 20 Katika uwanja wa Malabo.

Mchezaji wa Guinea, Kevin Constant (kshoto) na mchezaji wa Cote d'Ivoire Yaya Touré (kulia).
Mchezaji wa Guinea, Kevin Constant (kshoto) na mchezaji wa Cote d'Ivoire Yaya Touré (kulia). REUTERS/Amr Abdallah Dalsh
Matangazo ya kibiashara

Cote d'Ivoire ilijitahidi kusawazisha wakati ambapo ilikua ikiburuzwa kwa bao 1-0 katika kipindi cha kwanza. Cote d'Ivoire ilishindwa kufanya vizuri wakati ambapo ilikua imepewa nafasi kubwa ya kushinda. Guinea, wenyewe, wamesema kuridhishwa na matokeo hayo.

Cote d'Ivoire ambayo imecheza ikiwa na wachezaji 10 dhidi ya kumi na mmoja wa Guinea, baada ya kufukuzwa kwa Gervinho, ilikuja juu, na kufaulu kufunga bao la kusawazisha, wakati ambapo Guinea ilikua ikiongoza kwa bao 1-0.

" Kitu muhimu hapa ni kuwa tumegawa alama, baada ya wachezaji kuchukua uamuzi katika kipindi cha pili", amesema Yaya Touré, nahodha wa timu ya taifa ya Cote d'Ivoire.

" Kwa kweli kulingana na idadi ya wachezaji kumi uwanjani hatukua na matumaini ya kufanya vizuri aidha kusawazisha katika mchuano huu. Nadhani wachezaji wa timu ya taifa ya Cote d'Ivoire wamekuwa mfano. Alama hii tuliyopata ni nzuri itatupelekea sisi kubadili mchezo katika mechi zitakazofuata"
, ameongeza Yaya Touré.

" Wakati wa mapumziko, tuliafikiana kwamba tunapaswa kubadili mchezo, kwani tumekua tumewapa nafasi kubwa wachezaji wa Guinea kuweza kutamba uwanjani”, ameeleza Kolo Touré.

Gervinho : " Kadi nyekundu haikuwa inastahili"

Hatimaye, mchezaji aliyekuwa mwenye bahati mbaya, katika mchuano wa kwanza wa Jumanne Januari 20, uliyochezwa katika uwanja wa Malabo, ni Gervinho, ambae alipewa kadi nyekundu baada ya kumpa kibao mchezaji wa Guinea, Naby Keita.

Hata hivyo Gervihno amejitetea akisema kwamba hakua na nia ya kumpiga kibao mchezaji huyo wa Guinea, bali alitaka kumkataza kwa mkono kutorejekea kosa alillofanya dhidi yake baada ya kukanyagwa mguuni. Lakini Gervinho amesema ameridhishwa na matokeo ya mechi, huku akikosoa hatua ya muamuzi ya kumuonyesha kadi nyekundu, ambayo ilimkosesha kuendelea na mchezo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.