Pata taarifa kuu

Pakistani: Shehbaz Sharif achaguliwa kuwa Waziri Mkuu na Bunge la taifa

Shehbaz Sharif amechaguliwa kuwa Waziri Mkuu wa Pakistan na Bunge la taifa leo Jumapili, Machi 3, kufuatia uchaguzi uliopita wa wabunge, ambao matokeo yake yalipingwa vikali na wafuasi wa Imran Khan.

Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa ya Ulaya huko Geneva mnamo Januari 9, 2023.
Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa ya Ulaya huko Geneva mnamo Januari 9, 2023. AP - Salvatore Di Nolfi
Matangazo ya kibiashara

Shehbaz Sharif, 72, ambaye alikuwa mkuu wa serikali kuanzia mwezi Aprili 2022 hadi mwezi Agosti 2023, amechaguliwa kwa kura 201 dhidi ya 92 za Omar Ayub Khan, mgombea anayeungwa mkono na Waziri Mkuu wa zamani Imran Khan, wiki tatu baada ya uchaguzi wa Februari 8, uliogubikwa na kasoro nyingi, linaripoti shiruka la habari la AFP.

Akiwa jela tangu mwezi Agosti na kuhukumiwa vifungo vizito, Imran Khan anadai kuwa uchaguzi huo ulivurugwa kihuni, kwa mpango wa jeshi lenye nguvu, ili kuzuia chama chake kurejea madarakani.

Hakuna waziri mkuu aliyekaa kwa miaka mitano

Ili kurejea madarakani, Shehbaz Sharif na chama chake, Pakistan Muslim League (PML-N), ilibidi wahitimishe makubaliano ya muungano na mpinzani wao wa kihistoria, Pakistan People's Party (PPP) cha Bilawal Bhutto Zardari, na vyama vingine kadhaa vidogo. Kwa upande wake, Rais wa zamani Asif Ali Zardari (2008-2013), mume wa Waziri Mkuu wa zamani aliyeuawa Benazir Bhutto na babake Bilawal, aliteuliwa na PPP kama mgombea wa pamoja katika uchaguzi wa urais.

Kikao cha bunge cha Jumapili kilikuwa chenye mvuto na kiligubikwa na majibizano ya udukuzi na wafuasi wa Imran Khan maarufu sana, aliyemtangulia Shehbaz Sharif kama waziri mkuu kati ya 2018 na 2022, kabla ya kuondolewa madarakani kwa bunge kutokuwa na imani naye. Shehbaz Sharif ambaye ni ndugu mdogo wa Nawaz Sharif, ambaye mwenyewe aliwahi kuwa waziri mkuu mara tatu, anatarajiwa kuapishwa siku ya Jumatatu kwa muhula wa miaka mitano. Hakuna waziri mkuu nchini Pakistan ambaye amewahi kutimiza miaka mitano madarakani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.