Pata taarifa kuu

Korea Kaskazini yarusha makombora mawili ya balestiki na kutishia jirani yake Korea Kusini

Korea Kaskazini imerusha makombora mawili ya balistiki na kufanya mashambulio ya nyuklia dhidi ya Korea Kusini usiku wa Jumatano kuamkia Alhamisi. Hili ni jibu la Pyongyang kwa siku 11 za mazoezi ya kijeshi ya Seoul na Washington ambayo yanamalizika Alhamisi hii, Agosti 31. 

Korea Kaskazini yarusha makombora mawili ya balistiki juu ya anga ya Korea Kusini Jumatano Agosti 30, 2023.
Korea Kaskazini yarusha makombora mawili ya balistiki juu ya anga ya Korea Kusini Jumatano Agosti 30, 2023. AP - Ahn Young-joon
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu wa Seoul, Nicolas Rocca

Ndege za kivita ziliruka mara kadhaa katika mji mkuu wa Korea Kusini Alhamisi hii, Agosti 31. Tukio adimu ambalo linaashiria mvutano wa kijeshi katika pande zote za mpaka. Ikiwa ni mazoezi ya gwaride la kijeshi huko Seoul mwishoni mwa mwezi Septemba, mafunzo haya ya kijeshi hufanyika katika hali ya wasiwasi.

Vyombo vya habari vya serikali vimeeleza kwa kina mpango huo wa jibu  dhidi ya uwezekano wa mashambulizi ya Marekani, hata ikiwa ni pamoja na kukalia kwa mabavu eneo la Korea Kusini. Ishara mpya ya kuongezeka kwa mvutano kati ya Korea mbili.

Baada ya kurusha makombora mawili ya balestiki karibu usiku wa manane kwa saa za Pyongyang usiku wa Jumatano kuamkia Alhamisi, Korea Kaskazini imetangaza majibu yake kwa"mazoezi ya kijeshi ya Korea Kusini" katika vyombo vya habari vya serikali. Chini ya uangalizi wa Kim Jong-un, Jeshi la Wananchi limefanya mashambulio ya kimbinu ya nyuklia na kutangaza mipango yake ya kuikalia baadhi ya maeneo ya Korea Kusini iwapo kutatokea shambulio lolote.

Mvutano huu unakuja saa chache baada ya kutumwa kwa ndege za kijeshi za Marekani B1-B kama sehemu ya mazoezi ya pamoja na Korea Kusini ambayo yanakamilika Alhamisi hii. Pyongyang inabaini kuwa haya ni mazoezi ya kila mara kwa ajili ya uvamizi wa eneo lake.

Mvutano unaendelea kuongezeka kati ya Korea mbili, ambazo zinatuhumiana kila upande kuwa karibu na washirika wake. Washington imesema Korea Kaskazini na Urusi zinajadili kikamilifu mkataba wa kuipa silaha Moscow kuhusiana na vita nchini Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.