Pata taarifa kuu

Mvua kubwa yaua watu kadhaa kusini-magharibi mwa Japan

Baada ya wiki moja ya mvua kubwa, maporomoko ya ardhi yamesababisha vifo vya watu kadhaa kusini magharibi mwa Japan siku ya Jumatatu. Serikali imewataka baadhi ya watu kuondoka katika maeneo yaliyo hatarini zaidi.

Maporomoko mengine ya ardhi katika eneo la Kurume, mkoani Fukuoka, yalisomba watu kumi, tisa kati yao walinusurika. Lakini kifo cha mtu mwenye miaka zaidi ya 70 kimethibitishwa, afisa wa kutoa misaada katika jiji hili ameliambia shirika la habari la AFP.
Maporomoko mengine ya ardhi katika eneo la Kurume, mkoani Fukuoka, yalisomba watu kumi, tisa kati yao walinusurika. Lakini kifo cha mtu mwenye miaka zaidi ya 70 kimethibitishwa, afisa wa kutoa misaada katika jiji hili ameliambia shirika la habari la AFP. AP - 104710+0900
Matangazo ya kibiashara

Idadi hii ya vifo huenda ikaongezeka, kutokana na mvua nyingine inayotarajiwa. Lakini angalau watu wawili walifariki katika mvua kubwa iliyonyesha Jumatatu Julai 10 kusini magharibi mwa Japan.

Baada ya wiki moja mvua kunysha bila kukata, mvua "kubwa" zaidi "kuwahi kurekodiwa katika eneo hilo", kulingana na mamlaka ya hali ya hewa nchini Japani, imesababisha mito kupasuka kingo zake. Ardhi hiyo iliyojaa udongo ilibomoka katika maporomoko ya ardhi, ambayo moja lilimuua mwanamke mwenye umri wa miaka 77 usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu. Nyumba ya mwanamku huyu ilimezwa na maporomoko ya udongo katika eneo la Saga, wazima moto wa eneo hilo wameliambia shirika la habari la AFP. Mumewe alipatikana akiwa hai na kupelekwa hospitalini.

Maporomoko mengine ya ardhi katika eneo la Kurume, mkoani Fukuoka, yalisomba watu kumi, tisa kati yao walinusurika. Lakini kifo cha mtu mwenye miaka zaidi ya 70 kimethibitishwa, afisa wa kutoa misaada katika jiji hili ameliambia shirika la habari la AFP. Vyombo vya habari vya ndani vilitangaza idadi kubwa zaidi ya watu waliofariki, huku shirika la habari la Kyodo likiripoti kuwa takribani watu watano walifariki siku ya  Jumatatu usiku.

Viwango kadhaa vya tahadhari

Mwili wa mtu mwingine uligunduliwa Kurume, karibu na mto uliofurika, kwa mujibu wa kituo cha televisheni cha NHK na Gazeti la Yomiuri Shimbun. Huko Hirokawa, katika mkoa huo wa Fukuoka, mwili wa mzee ulipatikana ndani ya gari lililojaa maji likiwa limenaswa kwenye mfereji wa umwagiliaji, kulingana na Gazeti la Yomiuri.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.