Pata taarifa kuu

China: Watu sita wakiwemo watoto watatu wameuawa katika shambulio la kisu

Nairobi – Watu sita wakiwemo watoto watatu wameuawa katika shule ya chekechea kwa kudungwa visu katika jimbo la Guangdong kusini mashariki mwa China.

Watu kadhaa wameuawa, wakiwemo watoto, katika shambulio la shule ya chekechea kusini mwa China
Watu kadhaa wameuawa, wakiwemo watoto, katika shambulio la shule ya chekechea kusini mwa China © Noel Celis, AFP
Matangazo ya kibiashara

Polisi wamesema wamemkamata mwanamume mwenye umri wa miaka 25 kwa jina la Wu katika mji wa Lianjiang kwa kuhusika na shambulio hilo.

Wahasiriwa wengine ni mwalimu na wazazi wawili, kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa afisa wa eneo hilo. Mtu mmoja pia amejeruhiwa.Polisi wametaja tukio hilo kama "shambulio la kukusudia."

Shambulio hilo lilitokea mapema leo Jumatatu wakati wazazi walipokuwa wakiwapeleka watoto wao kwa ajili ya masomo.

Silaha za moto zimepigwa marufuku nchini China lakini nchi hiyo imeshuhudia mashambulio mengi ya visu katika miaka ya hivi karibuni, ingawa pia kulikuwa na tukio moja ambapo mshambuliaji alitumia dawa ya kemikali kujeruhi  watoto 50 waliokuwa darasani.

Mwezi Agosti mwaka jana, mshambuliaji mwenye kisu alivamia shule ya chekechea katika mkoa wa Jiangxi kusini-mashariki wa China na kuua watu watatu na kujeruhi wengine sita.

Mnamo Aprili 2021, watoto wawili walikufa huku wengine 16 wakijeruhiwa wakati wa shambulio la watu wengi katika mji wa Beiliu, katika mkoa unaojitawala wa Guangxi Zhuang.

Oktoba 2018, watoto 14 walijeruhiwa katika shambulio la kisu katika shule ya chekechea huko Chongqing, kusini-magharibi mwa China.

Katika visa hivi vingi, wahusika ni wanaume na wameonyesha chuki dhidi ya jamii. Mitindo kama hiyo imeonekana katika mauaji ya watu wengi katika nchi nyingine, kutoka Marekani hadi Japani. Lakini wataalam wanasema kunaweza kuwa na sababu za ziada za ongezeko la wazi la kuchomwa visu nchini China.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.