Pata taarifa kuu
DIPLOMASIA-USHIRIKIANO

Yellen ana matumaini kuhusu uhusiano na China baada ya ziara yake Beijing

Uhusiano kati ya Marekani na China sasa una "misingi imara zaidi", Waziri wa Fedha wa Marekani Janet Yellen amesema leo Jumapili, akiwa na matumaini baada ya ziara ya siku nne mjini Beijing yenye lengo la kupunguza mvutano kati ya mataifa hayo mawili yenye nguvu zaidi duniani.

Waziri wa Fedha wa Marekani Janet Yellen na Naibu Waziri Mkuu He Lifeng wanakutana Beijing Julai 8, 2023.
Waziri wa Fedha wa Marekani Janet Yellen na Naibu Waziri Mkuu He Lifeng wanakutana Beijing Julai 8, 2023. © Mark Schiefelbein/AFP
Matangazo ya kibiashara

Alipowasili katika mji mkuu wa China siku ya Alhamisi, Bi Yellen alipokelewa na maafisa kadhaa wakuu wa serikali, akiwemo Waziri Mkuu Li Qiang, na kuendelea kuomba mazungumzo na ushirikiano zaidi licha ya tofauti hizo.

"Kwa ujumla, ninaamini kwamba mikutano yangu ya nchi mbili - ambayo ilichukua jumla ya masaa kumi kwa siku mbili - ni hatua ya iliyopigwa katika juhudi zetu za kuanzisha uhusiano kati ya Marekani na China katika misingi thabiti zaidi," amesema katika mkutano na waandishi wa habari katika Ubalozi wa Marekani mjini Beijing leo Jumapili.

Ziara hii, ambayo ni ya kwanza kwa Bi. Yellen tangu aingie madarakani mwaka wa 2021, inakuja wiki chache baada ya ile ya Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken na kuashiria nia ya utawala wa Biden kuleta utulivu wa uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

"Mataifa yote mawili yana wajibu wa kusimamia uhusiano huu kwa kuwajibika: kutafuta njia ya kuishi pamoja na kushiriki ustawi wa kimataifa," Waziri wa Fedha wa Marekani amesema, akisisitiza umuhimu "mkubwa" wa mawasiliano ya ngazi ya juu.

Tunaamini dunia ni kubwa kwa nchi zetu mbili kuweza fanikisha.

Ingawa hakuna maendeleo makubwa ambayo yametangazwa, shirika la habari la serikali la Xinhua limesisitiza kwamba mkutano wa Jumamosi kati ya Bi Yellen na Naibu Waziri Mkuu He Lifeng umewezesha kukubaliana juu ya "kuimarishwa kwa mawasiliano na ushirikiano ili kukabiliana na changamoto za kimataifa".

- 'Mvutano mkubwa' -

Waziri wa Fedha wa Marekani amekiri kwamba kuna "kutoelewana kwa kiasi kikubwa" kati ya nchi hizo mbili, lakini amehakikisha kuwa majadiliano ya Beijing yalikuwa "ya moja kwa moja, makubwa na yenye tija".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.