Pata taarifa kuu

China: Waziri wa Fedha wa Marekani kuzuru Beijing wiki hii

Baada ya Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken, Waziri wa Fedha wa Marekani Janet Yellen atasafiri kwenda China kuanzia Alhamisi hadi Jumapili wiki hii kukutana na maafisa wa China, wizara hiyo ilisema siku ya Jumapili. Hii ni ziara mpya ya Marekani nchini China.

Waziri wa Fedha wa Marekani Janet Yellen.
Waziri wa Fedha wa Marekani Janet Yellen. AP - Manuel Balce Ceneta
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa fedha wa Marekani anatarajia kukutana na serikali ya China ili kusimamia uhusiano kati ya China na Marekani "kwa uwajibikaji".

Wakati wa ziara yake mjini Beijing, Waziri wa Fedha atakutana na wajumbe wa serikali "juu ya umuhimu kwa nchi hizo mbili, kama nchi zinazoongoza kiuchumi duniani, kusimamia uhusiano [wao] kwa njia ya uwajibikaji", kulingana na Wizara Fedha.

Janet Yellen pia ana nia ya kusisitiza juu ya haja ya "kuwasiliana moja kwa moja juu ya masuala ya wasiwasi na kufanya kazi ili kukabiliana na changamoto za kimataifa".

"Hatutarajii mafanikio makubwa [katika mahusiano kati ya nchi hizi mbili] kufuatia ziara hii," afisa kutoka Wizara ya Fedha amesema. "Hata hivyo, tunatarajia kuwa na majadiliano yenye kujenga na kuanzisha njia za mawasiliano za muda mrefu" na China, ameongeza afisa huyo.

Mivutano ya mara kwa mara

Uhusiano wa kidiplomasia na kiuchumi kati ya nchi hizo mbili umezorota taratibu tangu kipindi cha Donald Trump.

Mnamo mwezi Novemba, rais wa Marekani Joe Biden alikutana na rais wa China Xi Jinping kwa mara ya kwanza ana kwa ana kujaribu kupunguza mvutano.

Katikati ya mwezi Juni, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alikwenda Beijing na kupokelewa na rais wa China, ishara iliyotafsiriwa kama maendeleo ya kidiplomasia.

Lakini wakati wa mkutano wa kampeni huko California mwishoni mwa mwezi Juni, Joe Biden alimwita Xi Jinping "dikteta", matamshi yaliyochukuliwa na Beijing kuwa "uchochezi".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.