Pata taarifa kuu

Korea Kaskazini kurusha makombora: Marekani, Japan na Korea Kusini kupeana taarifa

Marekani na washirika wake wawili wa Asia, Japan na Korea Kusini, watapeana taarifa kuhusu kurushwa kwa makombora ya Korea Kaskazini. Tangazo hili limetolewa baada ya mkutano wa mawaziri wa ulinzi wa nchi hizi nchini Singapore ambapo mkutano wa kilele wa usalama wa Shangri-La unafanyika.

Waziri wa Ulinzi Lee Jong-sup (kushoto) na Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin (kulia) wakiwa katika Mkutano wa Usalama wa Shangri-La.
Waziri wa Ulinzi Lee Jong-sup (kushoto) na Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin (kulia) wakiwa katika Mkutano wa Usalama wa Shangri-La. AP - Vincent Thian
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Tokyo, Frédéric Charles

Tangu kuongezeka kwa uhusiano kati ya Japan na Korea Kusini, Marekani imeimarisha muungano wake wa kijeshi na washirika wake wawili kutokana na vitisho vya Korea Kaskazini, China na Urusi.

Marekani, Japan na Korea Kusini zitapeana data za wakati halisi "ili kuboresha uwezo wa kila nchi wa kugundua na kutathmini makombora yaliyorushwa na Korea Kaskazini". Tangazo hili linafuatia jaribio la Pyongyang la kurushwa bila mafanikio siku chache zilizopita satelaiti ya kijasusi kinyume na maazimio ya Umoja wa Mataifa. Kwa muda wa mwaka mmoja, Korea Kaskazini imezidisha majaribio ya makombora ya balestiki na kujitangaza kuwa nchi nchi yenye nguvu za nyuklia.

Maridhiano kati ya Japan na Korea Kusini baada ya miaka mingi ya mizozo yanaifanya Marekani kuchukua hatua za kuufanya muungano wake kuwa wa kisasa na kuimarisha uzuiaji na washirika wake wawili muhimu zaidi barani Asia. Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin anasema nchi hizo tatu zinakabiliwa na changamoto zinazofanana "zinazohusiana na tabia ya kulazimisha ya China, chokochoko hatari za Korea Kaskazini, na vita vya kikatili vilivyochaguliwa na Urusi nchini Ukraine."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.