Pata taarifa kuu

Shambulio la mtandaoni: China yaishutumu Marekani na washirika wake kwa 'habari potofu'

China imeishutumu Marekani na washirika wake wanne wa Magharibi kwa kujihusisha na "kampeni ya kupotosha habari" baada ya kutolewa kwa ripoti inayodai kuwa Beijing imefadhili mashambulizi ya mtandaoni dhidi ya maslahi yao.

Inadaiwa kuwa wadukuzi wamejipenyeza kimya kimya kwenye "miundombinu muhimu" ya Marekani.
Inadaiwa kuwa wadukuzi wamejipenyeza kimya kimya kwenye "miundombinu muhimu" ya Marekani. © Pixabay/Geralt
Matangazo ya kibiashara

"Hii ni ripoti ambayo ina dosari kubwa na isiyo ya kitaalamu," Mao Ning, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, amesema wakati wa mkutano na waandishi wa habari.

"Ni wazi kuwa hii ni kampeni ya pamoja ya kutoa taarifa potofu na nchi za muungano wa Macho Matano "Five Eyes", iliozinduliwa na Marekani kwa madhumuni ya kisiasa ya kijiografia," ameongeza.

Muungano wa "Macho Matano" ni mtandao shirikishi wa kijasusi unaojumuisha Australia, Marekani, Canada, Uingereza na New Zealand - nchi ambazo mara nyingi zina mizozo na China, kwa viwango tofauti.

Katika ushauri wa pamoja, mamlaka katika nchi hizi zimeonya kuhusu "kundi ovu lenye shughuli" linalohusishwa na "mhusika mtandaoni anayefadhiliwa na serikali kutoka Jamhuri ya Watu wa China, pia anajulikana kama Volt Typhoon. ".

Inadaiwa kuwa wadukuzi wamejipenyeza kimya kimya "miundombinu muhimu" ya Marekani.

"Kama inavyojlikana na kila mtu, Muungano wa Macho Matano ndio shirika kubwa zaidi la kijasusi duniani na Shirika la Usalama wa Taifa (NSA) ndilo shirika kubwa zaidi la udukuzi duniani," Mao Ning amesema.

"Ukweli kwamba wanaungana kuchapisha ripoti kama hiyo ya upotoshaji yenyewe ni ya kejeli."

NSA, ambayo mara nyingi hushutumiwa na Beijing, ilijulikana na mmoja wa wanasayansi wake wa zamani wa kompyuta, Mmarekani Edward Snowden, ambaye alifichua kuwepo kwa mfumo wa Marekani wa ufuatiliaji wa kimataifa wa mawasiliano na hasa mtandao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.