Pata taarifa kuu

Vietnam: Mwandishi wa habari wa kujitegemea ahukumiwa kifungo cha miaka sita jela

Nguyen Lan Thang, mwanablogu na mwanaharakati maarufu wa Kivietinamu, alihukumiwa Jumatano (Aprili 12) kifungo cha miaka sita jela, baada ya mahakama ya Hanoi kumpata na hatia kwa propaganda dhidi ya utawala wa kikomunisti, kesi ambayo ilisikilizwa kwa faragha.

Mwanahabari, Nguyen Lan Thang alihukumiwa siku ya Jumatano Aprili 12 kifungo cha miaka sita jela.
Mwanahabari, Nguyen Lan Thang alihukumiwa siku ya Jumatano Aprili 12 kifungo cha miaka sita jela. AFP - HOANG DINH NAM
Matangazo ya kibiashara

Mwandishi wa habari, Nguyen Lan Thang anajulikana kwa kuripoti juu ya maandamano mengi na ukiukwaji wa haki za binadamu nchini mwake. Mashirika yasiyo ya kiserikali yamelaani shambulio jipya dhidi ya uhuru wa kujieleza na kutaka aachiliwe mara moja baada ya kesi yake kushughulikiwa haraka na kudumu kwa siku moja tu. Kesi hiyo ilifanyika kwa faragha, mbele ya mke wa mshtakiwa tu na wanasheria.

Mwanahabari huyo mwenye umri wa miaka 48 ambaye alikamatwa mwezi Julai 2022, alihukumiwa kifungo kikubwa kwa kurusha kwenye mitandao ya kijamii video zilizopigwa katika maandamano ya kuunga mkono mazingira. Nguyen Lan Thang, mwandishi wa zaidi ya makala 130 kwenye blogu yake, mshiriki wa muda mrefu wa Radio Free Asia, ametetea bila kuchoka haki za binadamu, uhuru wa dini na kukemea aina zote za dhuluma. Alitembelea maeneo ya unyakuzi wa ardhi kwa lazima ili kurekodi matumizi ya nguvu kupita kiasi na mamlaka na pia alishiriki katika maandamano mengi ya kuunga mkono mazingira, kulingana na shirika la kimataifa la kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch.

Mwanablogu huyo alihukumiwa chini ya Kifungu cha 117 cha Kanuni ya Adhabu ya Vietnam, ambacho kinatoa adhabu kali zaidi ambayo serikali inaweza kutoa kwa wapinzani, ambayo ni mashtaka ya "kufanya propaganda dhidi ya serikali". Vietnam kwa miaka mingi imeweka vikwazo vikali kwa uhuru wa kujieleza, hasa dhidi ya waandishi wenye wafuasi wengi wa mitandao ya kijamii, ambao hunyamazishwa mara moja na kutupwa jela. Na vyombo vya habari vay kibinafsi pia vimepigwa marufuku.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.