Pata taarifa kuu

Korea Kaskazini yarusha kombora la masafa marefu na kuzua wasiwasi wa kiusalama

NAIROBI – Korea Kaskazini imerusha kombora lake ambalo linaelezwa limefika katika êneo la bahari karibu na Japan, na kuzua wasiwasi wa kiusalama wa kikanda.


Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong Un
Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong Un AP
Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa Majeshi nchini Korea Kusini amethibitisha kurushwa kwa kombora hilo lenye nguvu, ambalo ripoti zinasema limetokea karibu na mji mkuu Pyongyang.

Kombora hilo linaripotiwa kuwa, limekwenda umbali wa Kilomita 1000 na kuanguka katika Bahari upande wa Japan, kitendo ambacho nchi hiyo imesema ni uchokozi.

Japan imesema iko katika tahadhari ya kiusalama, baada ya kuthibitisha kufika kwa kombora hilo katika êneo lake la bahari lakini, haikuleza ni wapi hasa ilikoangukia.

Marekani nayo imelaani  kitendo hicho cha Korea Kaskazini, inachosema Pyongyang inaendelea kuzua wasiwasi wa kikanda.

Msemaji wa Baraza la Usalama, Adrienne Watson amesema rais Joe Biden na washauri wake kuhusu masuala ya usalama wanathathmini hatua hiyo ya Korea Kaskazini, ambayo amesema ni kinyume cha azimio la Baraza la Usalama wa Kimataifa.

Tangu kuanza kwa mwaka huu Korea Kaskazini imeendelea kujaribu makombora yake ya masafa marefu na karibu, suala ambalo linatishia usalama wa kikanda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.