Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

India: Wanne wauawa kwa kupigwa risasi kwenye kambi ya kijeshi ya Punjab

Watu wanne wameuawa katika tukio la shambulio liliotokea Jumatano alfajiri Aprili 12 katika kambi ya kijeshi kaskazini mwa India, jeshi la India limetangaza. Tukio hili liliripotiwa mwendo wa saa 10:35 asubuhi katika kituo cha Bathinda huko Punjab, ambapo mvutano ni mkubwa kati ya kuibuka tena kwa vuguvugu linalotaka kujitenga la Sikh, shirika la habari la AFP limeripoti.

Vikosi vya usalama vya India vimezingira kituo cha polisi ambapo magaidi wasiojulikana wamekimbilia katika mji wa Gurdaspur huko Punjab.
Vikosi vya usalama vya India vimezingira kituo cha polisi ambapo magaidi wasiojulikana wamekimbilia katika mji wa Gurdaspur huko Punjab. REUTERS/Munish Sharma
Matangazo ya kibiashara

"Eneo hilo bado limefungwa na uchunguzi wa pamoja na polisi wa Punjab unaratibiwa kubaini ukweli," jeshi la India limesema katika taarifa. Afisa mkuu wa polisi wa Bathinda G.S. Khurana amekiambia kituo cha NDTV kwamba tukio hilo halikuonekana kuwa shambulio la kigaidi.

Hali ya mvutano

Polisi wa jimbo na Wizara ya Ulinzi ya India hawakujibu maombi kutoka kwa shirika la habari la aAFP. Hali kwa sasa ni ya wasiwasi huko Punjab ambapo mamlaka imekuwa ikifuatilia bila mafanikio mhubiri anayetaka kujitenga kwa eneo moja la nchi hiyo, Amritpal Singhpar tangu mwezi uliopita.

Akiwa na umri wa miaka 30, Amritpal Singh amejijengea jina katika miezi ya hivi karibuni kwa kutaka kuundwa kwa Khalistan, jimbo linalodaiwa na wanaharakati wa Sikh huko Punjab, ambao mapambano yao yalizua vurugu katika miaka ya 1980 na 1990 na kusababisha maelfu ya watu kuuawa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.