Kumi na moja wafariki na wengi hawajulikani waliko kufuatia maporomoko ya udongo Indonesia
Watu kumi na moja wamefariki na wengine 50 hawajilikani walipo Jumatatu, Machi 6, baada ya mvua kubwa kunyesha na maporomoko ya ardhi kuripotiwa kwenye Visiwa vya Riau, eneo lililo mbali na mji ni kati ya mbali zaidi katika visiwa vya Indonesia, imesema idara ya majanga ya asili,kulingana na shirika la habari la AFP.
Imechapishwa:
Mvua kubwa imesababisha maporomoko ya udongo nchini Indonesia. Angalau watu kumi na moja wameangamia na wengine 50 hawajulikani waliko, baada ya mvua kubwa na maporomoko ya udongo kwenye moja ya visiwa vya mbali zaidi katika visiwa vya Indonesia, shirika la kitaifa linalosimamia majanga ya asili lilmesema.
Janga hilo lilitokea kwenye Visiwa vya Riau, msemaji wa Shirika la majanga asilia, Abdul Muhari, mesema kwenye kituo cha runinga.