Pata taarifa kuu

Korea Kusini: Maombolezo ya kitaifa baada ya tukio la Halloween

Korea Kusini inaomboleza vifo vya watu 153 waliokufa katika mkanyagano wakati wa sherehe za Halloween, mjini Seoul, Korea Kusini. Katika eneo la mkasa, rais wa Korea Kusini ametangaza maombolezo ya kitaifa.

Watu wakiweka shada za maua ili kuwaenzi wahanga karibu na eneo la ajali mbaya huko Seoul, Korea Kusini, Jumapili, Oktoba 30, 2022, kufuatia sherehe za Jumamosi usiku za Halloween.
Watu wakiweka shada za maua ili kuwaenzi wahanga karibu na eneo la ajali mbaya huko Seoul, Korea Kusini, Jumapili, Oktoba 30, 2022, kufuatia sherehe za Jumamosi usiku za Halloween. AP - Ahn Young-joon
Matangazo ya kibiashara

Akiwasili kwenye eneo la mkasa, akiwa amevalia koti la kijani la maafisa wa idara ya huduma za dharura, Rais wa Korea Kusini Yoon Suk-yeol ametangaza maombolezo ya kitaifa na kuahidi kufunguliwa kwa uchunguzi "mkali" kuhusu mkanyagano huo. Kulingana na ripoti ya awali, takriban watu 153 walikufa, wakiwemo wageni 22 wa mataifa mbalimbali. Pia kuna makumi ya waliojeruhiwa. Miongoni mwa waliofariki, Mfaransa mmoja, Quai d'Orsay aimetangaza siku ya Jumapili. Raia wawili wa Ufaransa walijeruhiwa, lakini wako katika hali nzuri.

Hisia ni kali nchini Korea Kusini siku moja baada ya tukio hili la kutisha la mkanyagano ambalo lilitokea katika wilaya ya Itaewon. 

Kwa mujibu wa vyombo vya usalama nchini humo, hili ni tukio baya zaidi kuwahi kutokea, ambapo rais Yoon Suk-Yeol, ameapa uchunguzi wa kina kufanyika kubaini kiini cha tukio.

Tukio hili kwenye wilaya ya Itaewon, linakadiriwa kuhudhuriwa na watu zaidi ya laki 1 wengi wao wakiwa vijana walio na umri wa chini ya miaka 20, ambapo walijitokeza kusherehekea Haloween.

Rais Yoon, ametangaza maombolezo ya kitaifa akilitaja tukio hilo kama doa kwa nchi yake, akitoa pole kwa familia zilizopoteza ndugu.

Viongozi wa dunia akiwemo kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis, wametuma salamu za pole kwa raia wa Korea Kusini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.