Marekani yaionya Urusi kuwa itakabiliwa vikali ikitumia silaha za maangamizi dhidi ya Ukraine
Marekani kwa mara nyingine, imeionya Urusi kuwa itakabiliwa vikali, iwapo itatumia silaha za nyuklia kuishambulia Ukraine.
Imechapishwa:
Wiki iliyopita, rais Vladimir Putin alionya kutumia kila mbinu ikiwemo silaha za nyuklia kuwalinda watu wake, huku akitangaza kuongeza idadi ya wanajeshi kwenda nchini Ukraine.
Wakati huo huo, zoezi la kura ya maoni ya kutaka maeneo yanayodhibitiwa na wanajeshi wa Moscow Mashariki na Kusini mwa Ukraine kuwa sehemu ya Urusi, linaendelea.
China na India zatoa wito kwa mazungumzo ya kumaliza vita nchini Ukraine
Watu katika eneo la Dagestan nchini Urusi wamekabiliana na polisi katika maandamano ya hivi punde kupinga hatua ya Urusi ya kusajili wanajeshi 300,000 wa akiba.
Zaidi ya watu 100 walikamatwa wakati wa maandamano katika mji mkuu wa mkoa wa Makhachkala, OVD-Info, mfuatiliaji huru wa haki za binadamu wa Urusi alisema.
Wakati huo huo China na India zimetoa mwito wa mazungumzo ya kumaliza vita vya Ukraine, na kuashiria kupungua kwa uungaji mkono thabiti katika sera ya uvamizi kwa mshirika wa jadi Urusi.
Katika mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi amezitaka Urusi na Ukraine kuzuia mgogoro huo kuenea na kuathiri nchi zinazoendelea. Amesema suluhisho la msingi ni kushughulikia wasiwasi wa kiusalama wa pande zote na kuwa na muundo wa usalama wenye usawa, thabiti na endelevu. India kwa upande wake, ilisema kuwa inasimama katika msingi wa amani na kutoa wito wa mazungumzo na diplomasia kama suluhisho pekee.