Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine: Vita vya ardhini na katika vyombo vya habari vyapamba moto

Urusi imeapa kuendelea na mashambulizi nchini Ukraine mpaka malengo yake "yamefikiwa'. Kremlin imebaini kwamba jeshi la Urusi linashambulia kwa mabomu maeneo yaliyotekwa tena na Ukraine. Urusi inajaribu kurejesha udhibiti, wakati Kyiv imekuwa kwenye mashambulizi ya kukabiliana na mashambulizi kwa siku kadhaa na imetwaa tena miji muhimu.

Ukraine, Septemba 12, 2022: safu yamagari ya kijeshi ya Ukraine ya shambulio la viongozi wa kijeshi lililoongozwa mashariki mwa nchi, katika mkoa wa Kharkiv.
Ukraine, Septemba 12, 2022: safu yamagari ya kijeshi ya Ukraine ya shambulio la viongozi wa kijeshi lililoongozwa mashariki mwa nchi, katika mkoa wa Kharkiv. via REUTERS - UKRAINIAN ARMED FORCES
Matangazo ya kibiashara

Vyombo vya habari vimeendelea kutoa habari kuhusiana na vita vinavyoendelea kati ya pande zote mbili: kutangaza kilomita za mraba za ardhi iliyochukuliwa tena kwa upande wa Ukraine, ili kuhakikisha kuendelea kwa mashambulizi kwa upande wa Urusi.

Ukraine inasema imerejesha kwenye himaya yake kilomita 500 kutoka kwa Urusi, kusini mwa nchi na, kwa upande wa mashariki, inatangaza kurejesha "zaidi ya vijiji ishirini" katika kipindi cha saa 24, dhidi ya Urusi. "Ukombozi wa maeneo kutoka kwa wavamizi wa Kirusi unaendelea katika mikoa ya Kharkiv na Donetsk" (Mashariki), jeshi la Ukraine limesema asubuhi ya leo.

Mji wa Izium umetekwa tena na jeshi la Ukraine, Rais Volodymyr Zelensky alisema Jumapili jioni. Ni moja wapo ya miji muhimu iliyochukuliwa mashariki mwa nchi, katika mkoa wa Kharkiv, tangu kuanza kwa mashambulio haya makubwa yaliyozinduliwa na jeshi la Ukraine mnamo Septemba 6.

Volodymyr Zelensky anazidisha jumbe kwenye mitandao ya kijamii, akiwashukuru askari wake, akitangaza ushindi, akionyesha picha za bendera za Ukraine zilizopandishwa tena katika jiji hili au lile. Waziri wa Ulinzi, Oleksii Reznikov, alizungumza katika mahojiano (yaliyotolewa mnamo Septemba 10) na gazeti la Le Monde,  hatua ya tatu katika vita hivi. Alisema hatua ya kwanza ni vita vya kuzuia, ya pili ni utulivu katika maeneo ya kivita na ya tatu,ni majibu ya mashambulizi yaliyoendeshwa hasa kwa msaada wa silaha kutoka nje ya nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.