Pata taarifa kuu

Ukraine: Timu ya wataalam wa IAEA wawasili kwenye kituo cha nyuklia cha Zaporizhia

Ujumbe wa shirika la Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) umewasili Alhamisi, Septemba 1 kwenye kituo cha nyuklia cha Zaporizhia, baada ya kuzuiwa kwa saa kadhaa karibu kilomita ishirini kutoka eneo hilo, kutokana na mashambulizi mapya ya anga yaliyotokea Alhamisi asubuhi na ambayo Kyiv na Moscow kwa mara nyingine tena wamefutilia mbali kuhusika.

Picha ya setilaiti iliyotolewa na Maxar Technologies inayoonyesha moto wa msituni nje ya kituo cha nyuklia cha Zaporizhia, Jumatatu Agosti 29, 2022.
Picha ya setilaiti iliyotolewa na Maxar Technologies inayoonyesha moto wa msituni nje ya kituo cha nyuklia cha Zaporizhia, Jumatatu Agosti 29, 2022. via REUTERS - MAXAR TECHNOLOGIES
Matangazo ya kibiashara

Msafara mrefu uliobeba wakaguzi wa shirika la Umoja wa Mataifa umefika katika eneo ambalo wanajeshi wa Urusi wapo kwa idadi kubwa na chanzo cha Ukraine kinachofahamu ziara ya wakaguzi hao kimeliambia shirika la habari la Reuters kwamba ziara ya ujumbe huo "huenda ikawa fupi kuliko ilivyotarajiwa".

Kulingana na IAEA na kampuni ya nishati ya umma ya Ukraine Energoatom, msafara huo ulicheleweshwa kwa saa tatu Alhamisi hii asubuhi yapata kilomita ishirini kutoka kwenye kituo hicho cha nyuklia, katika kituo cha ukaguzi ambacho bado kinashikiliwa na wanajeshi wa Ukraine, hadi hali ilikapokuwa salama tena baada ya mashambulizi mapya ya anga yaliyotokea asubuhi karibu na eneo hilo.

Kituo cha nyuklia kitakachotembelewa na wakaguzi wa IAEA, kinachopatikana katika mji wa Enerhodar, karibu kilomita 120 kutoka mji wa Zaporizhia ambacho kilipewa jina lake, kilianguka chini ya udhibiti wa Urusi mapema mwezi Machi, muda mfupi baada ya uzinduzi wa mashambulizi nchini Ukraine, lakini kazi zoe kwenye kituo hiki zinasimamiwa na mafundi wa Ukraine.

Maeneo ya pembezoni mwa kituo hicho cha nyuklia yanakabiliwa na milipuko ya mara kwa mara kwa wiki kadhaa, ambayo Urusi na Ukraine wamefutilia mbali kuhusika, na kuchochea hofu ya janga la nyuklia na kusababisha nchi kadhaa na mashirika ya kimataifa kutaka kutengwa kwa eneo lisilo na kijeshi.

Kyiv na Moscow kwa mara nyingine tena wameshtumiana kila mmoja kwa kuhusika na milipuko hiyo iliyotokea Alhamisi asubuhi wakati ujumbe wa IAEA ulipokuwa ukielekea kwenye kituo hicho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.