Pata taarifa kuu

China: UN yashutumu 'uhalifu dhidi ya binadamu' unaowezekana dhidi ya Uyghurs

Katika ripoti iliyosubiriwa kwa muda mrefu iliyochapishwa siku ya Jumatano, Umoja wa Mataifa unatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua za haraka katika kukabiliana na tuhuma za mateso na unyanyasaji wa kingono katika eneo la China la Xinjiang ambazo shirika hilo linaona kuwa ni "za kuaminika". Nakala hiyo, ambayo pia inaibua uwezekano wa "uhalifu dhidi ya ubinadamu", madai ambayo yameamsha hasira ya Beijing.

Watu kutoka jamii ya Uyghur, ambao wengi wao ni Waislamu, wakiwa chini ya amri ya viosi vya usalamakatika mitaa ya Kashgar, Xinjiang, Machi 23, 2017.
Watu kutoka jamii ya Uyghur, ambao wengi wao ni Waislamu, wakiwa chini ya amri ya viosi vya usalamakatika mitaa ya Kashgar, Xinjiang, Machi 23, 2017. REUTERS/Thomas Peter
Matangazo ya kibiashara

Ripoti iliyokuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu ya Umoja wa Mataifa kuhusu eneo la Xinjiang nchini China, iliyochapishwa Jumatano Agosti 31, inaibua uwezekano wa "uhalifu dhidi ya ubinadamu" na inataja "ushahidi wa kuaminika" wa mateso na unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya watu wa jamii ya Uyghur walio wachache na kutoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua haraka.

"Kiwango cha visa vya kuzuiliwa kiholela na ubaguzi kwa watu wa jamii ya Uyghurs na makundi mengine yenye Waislamu wengi […] kinaweza kuwa uhalifu wa kimataifa, hasa uhalifu dhidi ya ubinadamu," imesema ripoti hiyo yenye kurasa hamsini katika hitimisho lake.

“Madai ya kuteswa mara kwa mara au kutendwa vibaya, kutumiwa vibaya, hasa kuhudumiwa vibaya kimatibabu na hali mbaya gerezani, yanaaminika, kama vile madai ya unyanyasaji wa kingono na kijinsia,” imeandika Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu.

Rais wa zamani wa Chile Michelle Bachelet, ambaye kwake ilikuwa siku ya mwisho kuhudumu kama Kamishna Mkuu baada ya muhula wa miaka minne, hivyo anatekeleza ahadi yake kwa kuruhusu waraka huo kuchapishwa muda mfupi kabla ya saa sita usiku huko Geneva.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.